WHO yaonya maambukizi mapya ya HIV na Vifo kuongezeka baada ya ARVs kusitishwa
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya maambukizi mapya ya HIV zaidi ya milioni 10 na vifo vya Watu milioni 3 vinavyohusiana na UKIMWI vinaweza kushuhudiwa kufuatia kusitishwa kwa msaada wa kigeni wa Marekani unaosaidia upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI, ARVs.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus WHO amesema hatua ya Marekani kujiondoa kusaidia mapambano ya HIV imeathiri usambazaji wa dawa katika nchi saba za Afrika, zikiwemo Kenya, Lesotho, Sudan Kusini, Burkina Faso, Mali, Nigeria, na Haiti, ambazo zinaweza kuishiwa dawa ndani ya miezi michache ijayo.
Dr. Tedros amesema kusitishwa kwa msaada huo wa Marekani kunaweza kufuta mafanikio ya miaka 20 katika kupambana na HIV huku pia akionya kuwa juhudi za kudhibiti magonjwa mengine kama polio, malaria, na kifua kikuu zimeathirika vibaya na ameiomba Marekani kuhakikisha kuwa inatoa muda wa mpito kwa nchi zilizoathirika ili ziweze kupata vyanzo mbadala vya fedha badala ya kusitisha msaada kwa ghafla, hatua ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya duniani.
Itakumbukwa Rais wa Marekani, Donald Trump alitangaza mwezi huu kusitisha kutoa fedha za misaada kupitia miradi iliyokuwa chini ya Shirika lake la misaada la USAID, hali iliyoibua taharuki hasa kwa nchi nyingi za Afrika zinazotegemea fedha za ufadhili kushughulika na magonjwa kama Ukimwi.
KARIBU DISCUSSION CORNER,WEKA COMMENT YAKO HAPA CHINI JUU YA MADA HII
#Afya News
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code