Ajali basi la mvungi,Watu 8 wapoteza Maisha wilayani Mwanga

Ajali basi la mvungi,Watu 8 wapoteza Maisha wilayani Mwanga

#1

Ajali basi la mvungi,Watu 8 wapoteza Maisha wilayani Mwanga



Watu nane wamefariki dunia na wengine 41 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Mvungi lenye namba za usajili T.222 DNL, aina ya Yutong, kupinduka na kutumbukia bondeni katika kijiji cha Mamba Msangeni, wilayani Mwanga, saa 12 asubuhi Aprili 3, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva aliyeshindwa kulimudu gari alipokuwa akijaribu kukwepa gari jingine kwenye kona kali. Basi hilo lilikuwa likitokea Ugweno kuelekea Dar es Salaam.

Majeruhi wa ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali, zikiwemo Hospitali ya Kifula, Hospitali ya Wilaya ya Mwanga, Hospitali ya KCMC Moshi, na Hospitali ya Mkoa wa Mawenzi.

Majina ya Waliopoteza Maisha

Mamlaka zimethibitisha vifo vya watu saba waliotambuliwa kuwa:

Ashura Omari Sakena (47) – Mkazi wa Vuchama, Mwanga

Zaituni Hashimu Mwanga (52) – Mkazi wa Masumbeni, Mwanga

Shabani Omari (62) – Mkazi wa Mwanga

Judith Saifoi Mwanga (43) – Mkazi wa Mangio, Mwanga

Hadija Omari (2) – Mkazi wa Mwanga

Haji Abubakar (50) – Mkazi wa Kilifi

Hamadi Hassani (64) – Mkazi wa Nagara, Ugweno

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mwanga kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Kwenye Orodha hii,Ameongezeka Mmoja,kwahyo mpaka Sasa waliopoteza Maisha ni Watu 8.

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code