Chanzo cha kifo,bondia wa Nigeria aliyeanguka kwenye pambano Ghana chagundulika

Chanzo cha kifo,bondia wa Nigeria aliyeanguka kwenye pambano Ghana chagundulika

#1

Chanzo cha kifo,bondia wa Nigeria aliyeanguka kwenye pambano Ghana chagundulika



Uchunguzi wa maiti(autopsy) uliyofanywa kwenye mwili wa bondia wa Nigeria, Segun ‘Success’ Olanrewaju, mwenye umri wa miaka 40, ambaye alianguka wakati wa pambano la ndondi kwenye uwanja wa Bukom Boxing Arena Jumamosi, Machi 29, 2025, umeonyesha kuwa alifariki kwa Sababu ya tatizo la moyo(Cardiac arrest).

Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu wa Taifa hilo na Afrika Magharibi, alikuwa akikabiliana na mzaliwa wa Accra John Mbanugu, aliyepewa jina la utani "Power" katika pambano hilo alipoanguka ghafla kwenye turubai katikati ya pambano, na kumfanya mwamuzi kuita mara moja msaada wa matibabu.  Wataalamu wa matibabu walikimbilia eneo la tukio lakini licha ya majaribio ya kumsaidia kwa haraka, bondia huyo mwenye umri wa miaka 40 ilisemekana ameshafariki.

Akitangaza matokeo ya uchunguzi wa maiti kwa waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Bodi ya Udhibiti wa Ndondi ya Nigeria na Rais wa Muungano wa Ndondi wa Afrika Magharibi, Remi Aboderin, alisema matokeo ya awali ya uchunguzi wa maiti yanaonyesha tatizo la Cardiac arrest kama chanzo cha kifo, lakini uchunguzi zaidi unahitajika kabla ya mwili huo kutolewa.

"Matokeo ya awali ya uchunguzi wa maiti yanaonyesha kuwa Segun alifariki kutokana na shida ya ghafla ya moyo au shida ya Cardiac arrest. Lakini uchunguzi zaidi wa hali ya moyo wake unahitajika, na kwa sababu hiyo, mwili wake hautatolewa Nigeria kwa mazishi hadi takriban wiki mbili," Aboderin alisema.

 Uchunguzi wa maiti ulifanyika Jumatano, Aprili 2 kufuatia amri ya mahakama kuhusu kifo cha bondia huyo wa Nigeria.

JOIN DISCUSSION [REPLY BELOW]


image quote pre code