Dhana hii imewadanganya Wengi"Kisukari ni ugonjwa wa wazee tu"

Dhana hii imewadanganya Wengi"Kisukari ni ugonjwa wa wazee tu"

#1

Dhana hii imewadanganya Wengi"Kisukari ni ugonjwa wa wazee tu"



Dhana hii imewadanganya Wengi"Kisukari ni ugonjwa wa wazee tu, hivyo kama uko chini ya miaka 40, huwezi kupata kisukari." Huna haja ya kujisumbua hata kupima

Ukweli: Kisukari aina ya pili kinapewa majina kama "ugonjwa wa wazee," lakini unaweza kutokea kwa mtu yeyote, ikiwemo vijana na watoto, hasa kutokana na mtindo wa maisha. Kisukari kinazidi kuwa changamoto kubwa kwa vijana wa kisasa, hasa kwa wale wanaokosa mazoezi na kula vyakula vyenye sukari nyingi.

"Watu wanene tu ndiyo hupata kisukari"
Ukweli: Hata watu wembamba wanaweza kupata kisukari, hasa aina ya pili.

Fahamu,historia ya familia yako inaweza kuongeza hatari ya wewe kupata Ugonjwa wa kisukari, ulaji wa vyakula vyenye sukari na mafuta kwa wingi, kutofanya mazoezi, unene kupita kiasi, msongo wa mawazo, na umri mkubwa. Vyote hivi huweza kuongeza hatari ya Mtu kupata Ugonjwa wa Kisukari.

#SOMA ZAIDI,Kuhusu Ugonjwa wa Kisukari,Chanzo,Dalili na Tiba

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code