Hatupo tayari kuona kwamba tunaishia hatua yarobo fainali kwa wakati huu

Hatupo tayari kuona kwamba tunaishia hatua yarobo fainali kwa wakati huu

#1

Hatupo tayari kuona kwamba tunaishia hatua yarobo fainali kwa wakati huu



UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwa namna yoyote watamlazimisha Mwarabu kuondoka katika hatua ya robo fainali kwa kupata matokeo chanya katika mchezo wa pili hatua ya robo fainali unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ili watinge nusu fainali.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita wa robo fainali baada ya dakika 90 ubao ulisoma Al Masry 2-0 Simba hivyo Simba inakibarua chakusaka mabao zaidi ya mawili katika mchezo wa nyumbani ambao utakamilisha dakika 180 za anga la kimataifa.

Mshindi wa jumla kwenye mchezo huo atatinga hatua ya nusu fainali na atakayepoteza safari yake itakuwa imegota mwisho huku mpinzani wa Simba, Al Masry akiwa ametanguliza mguu moja kuelekea nusu fainali.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu ila wapo tayari kuhakikisha wanamlazimisha Mwarabu kuondoka kwenye hatua ya robo fainali kwa kupata matokeo chanya.

“Hatupo tayari kuona kwamba tunaishia hatua yar obo fainali kwa wakati huu, tutamlazimisha Mwarabu kuodoka kwenye robo fainali kwa namna yoyote ile, tutampelekea pumzi ya moto kwa kuwa tupo nyumbani.

“Uwanja wa Benjamini Mkapa hatutaki kuona unapata aibu, tutakuwa nyumbani na tunahitaji kuona tunapata matokeo mazuri, Wanasimba hili linatuhusu wote ni lazima tuungane, tushirikiane kwani inawezekana na safari hii tunavuka.

“Kuelekea katika mchezo huu tunakusanya kila silaha yetu ili kwenda nusu fainali na tutamtumia kila Mwanasimba ili atoe mchango wake ambao utaiwezesha klabu kufika nusu fainali. Makosa yaliyotokea Misri yanafanyiwa kazi na benchi la ufundi.”

Reply


image quote pre code