MAAJABU:Mimba yatunga nje ya mfuko wa uzazi kwa miaka minne

MAAJABU:Mimba yatunga nje ya mfuko wa uzazi kwa miaka minne

#1

MAAJABU:Mimba yatunga nje ya mfuko wa uzazi kwa miaka minne







MKAZI wa Kijiji cha Mbika kata Ushetu Halmashauri ya Ushetu wilayani hapa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mayega (55) amefanyiwa upasuaji kuondoa kichanga kilichofia tumboni baada ya mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi kwa miaka minne.

Sophia alifanyiwa upasuaji huo wa kuongoa kichanga hicho baada ya mimba kutunga akiwa na miaka 51. 

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga, Augustino Maufi, alibainisha hayo wakati akizungumza na Nipashe baada ya kufanya upasuaji huo. 

Dk. Maufi, alisema walipokea mjamzito huyo kutoka Hospitali ya Manispaa ya Kahama, baada ya kumfanyia vipimo, walibaini  mimba ilikuwa imetunga nje ya mfuko wa kizazi badala ya kwenye mirija ya uzazi.

 Alisema zaidi ya miaka mitatu iliyopita, tumbo mjazito huyo lilikuwa limejaa, hivyo kutakiwa kufanyiwa upasuaji ili kuokoa maisha yake. 

Alisema wakati anachukua maelezo kutoka kwa mjamzito huyo, alidai miezi miwili ya kwanza alikuwa akisikia mapigo ya moyo ya mtoto tumboni baada ya hapo hakuna kilichokuwa kikiendelea. 

Dk. Maufi, alisema walipomfanyia kipimo cha ‘Utral Sound’ na X-ray vilibainisha kuwa ujauzito wake umetungwa nje ya kizazi na kwamba baada ya upasuaji walikuta mtoto amekwisha kufa. 

Alisema hali za mzazi huyo  kwa  sasa inaendelea vema na kuzidi kuimarika siku hadi siku. 

“Mimba ambazo huwa zinatungia kwenye yai nyingi huwa zinapasuka ndani ya miezi mitatu ya kwanza, ni mara chache kukua kuelekea kwenye hatua ya pili na ya tatu,” alisema Dk. Maufi na kuongeza kuwa: “ Kwa mgonjwa wetu tunashangaa mimba kukua hadi kufikia hatua hii, mara nyingi kukua ni changamoto na tunazozipata zinakuwa mtoto kafia tumboni.” 

Awali akieleza namna alivyokaa na ujauzito kwa kipindi chote hicho,  Sophia, alisema shida ilianza kwa  dalili kuonyesha kuwa ana mimba na wakati huo alikuwa na miaka 51. 

Alisema alikwenda  Hospitali ya Manispaa ya Kahama kufanyiwa vipimo, lakini ilibainika hakua na tatizo lolote. 

Alisema baada ya matatizo kuanza, alikwenda kwa mganga wa kienyeji kuchukua dawa na kuanza kutumia. 

 Kwa mujibu wa Sophia, aliacha kufuata huduma kwa mganga huyo baada ya kufariki dunia. 

Alisema baada ya hali yake kubadilika mara kwa mara, alipelekwa hospitalini hapo na kufanyiwa upasuaji ili kuokoa maisha yake kutokana na mtoto kufia tumboni.

Reply


image quote pre code