Matokeo Leo,Yanga yaifunga Tabora United 3-0
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi wamevuna pointi tatu ugenini kwenye mchezo dhidi ya Tabora United ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili msimu wa 2024/25.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Novemba 7 2024 ubao ulisoma Yanga 1-3 Tabora United ambao waliandika rekodi yakuwa timu iliyopata ushindi mkubwa mbele ya Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.
Mchezo wa leo Aprili 2 2025, ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi umesoma Tabora United 0-3 Yanga na bao la ufunguzi kwa Yanga limefungwa na beki Israel Mwenda dakika ya 20 kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 baada ya kiungo Maxi Nzengeli kuhama kimbinu kwenye eneo ambalo alisimama na kumpa nafasi Mwenda kupenyeza mpira uliozama nyavuni.
Prince Dube amefunga bao la tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tabora United anafikisha mabao 11 kwenye ligi akiwa ametoa jumla ya pasi 7 msimu wa 2024/25. Clement Mzize alifunga bao la pili dakika ya 57 likiwa ni bao lake la 11 ndani ya ligi akiwa namba moja kwa wenye mabao mengi ndani ya kikosi cha Yanga.
Yanga inafikisha jumla ya pointi 61 kwenye ligi na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 61 kibindoni ikiwa nit imu inayoongoza kwa kufunga mabao mengi ndani ya ligi na nyota wawili Mzize na Dube wote wametupia mabao 11 kila mmoja.
HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA KILICHOANZA
Kikosi kinachoanza kipo namna:-Djigui Diarra, Israel Mwenda, Boka, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Prince Dube, Pacome na Clement Mzize.
Wachezaji wa akiba ni Aweso ambaye ni kipa, Nickson Kibabage, Bakari Nondo, Kibwana Shomari, Dennis Nkane, Sure Boy, Farid Mussa na Ikanga Lombo Jonathan.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code