Miili sita ya wanakwaya wa Kanisa la KKKT Waliofariki kwa Ajali kuzikwa Leo

Miili sita ya wanakwaya wa Kanisa la KKKT Waliofariki kwa Ajali kuzikwa Leo

#1

Miili sita ya wanakwaya wa Kanisa la KKKT Waliofariki kwa Ajali kuzikwa Leo



Miili sita ya wanakwaya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Mmeni Chome, Dayosisi ya Pare waliofariki kwa ajali ya gari wilayani Same mkoani Kilimanjaro itazikwa leo Jumatano Aprili, 02, 2025.

Ajali hiyo ilitokea Machi 30, 2025 eneo la barabara ya Bangalala, wakati wanakwaya hao wakitokea Chome kuelekea Vudee kuinjilisha.

Gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Coaster lilikosa mwelekeo na kupinduka katika milima ya Pare na kusababisha vifo hivyo na majeruhi 23.

Watakaozikwa leo baada ya ibada itakayofanyika kwenye usharika wa Chome ni Namsifu Mbula (79), Mbazi Mjema (14), Paulo Mchome (40), Christina Kirumbi (60), Agness Mchome (59) na Niwaeli Ngeruya (74).

Miili ya wanakwaya hao iliagwa jana Aprili Mosi, 2025 katika kanisa kuu la KKKT, Dayosisi ya Pare.

Mkuu wa dayosisi hiyo, Askofu Charles Mjema akihubiri katika ibada ya kuaga miili hiyo amewataka wananchi kuishi maisha ya kujiandaa wakati wote na kuacha dhuluma.

“Katika maisha yetu hapa duniani tuishi kama tunaokufa sasa hivi, maana hatujui wakati wa bwana utafika lini. Tuache kuishi maisha ya kiholela, ya kujifikiria kuwa tutakaa hapa duniani, unajua wale wanaowadhulumu wenzao wanafanya hivyo kwa sababu wanafikiri wana maisha marefu, lakini unaweza ukamdhulumu leo na baadaye ukawa haupo.”

“Acha dhuluma, ndugu zangu, maisha yetu ni mafupi mno na kwa kuwa siri hii imefichwa hakuna anayejua muda na saa ya kuondoka duniani. Bwana anasema uwe tayari wakati unaofaa na usiofaa, tengeneza mambo yako ili ikitokea kuitwa ufie mikononi mwa Bwana,” alisema.

Askofu Mjema alikaririwa akisema wanakwaya hao walikuwa wanakwenda Usharika wa Vudee kutoa sadaka kwa ajili ya huduma za misioni.

“Wanakwaya hawa walikuwa wamealikwa kwa ajili ya kushiriki kutoa sadaka muhimu ya misioni. Ndani ya dayosisi yetu tuna sadaka ya misioni inayotumika kueneza injili katika maeneo yale ambayo kipato chao ni kidogo ili watumishi wanaotumika pale waweze kueneza injili,” amesema Askofu Mjema.

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code