Mwanamke achapisha bango na kuita jamii yake baada ya kuwa wa Kwanza kupanda Ndege kwenye jamii nzima
Mwanamke mmoja amechapisha bango na kuita jamii yake kusherehekea naye kwa kuwa "mwanamke wa kwanza kuingia kwenye ndege" katika jamii yake.
Mwanamke huyo amekuwa gumzo sana kwenye mitandao baada ya kusherehekea kuwa "mwanamke wa kwanza katika jamii yake kusafiri kupitia ndege."
Gold Ike aliingia kwenye ukurasa wa Facebook siku nne zilizopita ili kushiriki video yake akipiga picha mbele ya ndege.
Kisha, Jumapili, Aprili 6, alifanya Sherehe na kuwaalika watu wa jamii yake kusherehekea pamoja naye.
Pia alichapisha bango ambalo lilikuwa limeandikwa: "Mwanamke wa kwanza kuingia kwenye ndege katika jamii yangu".
Wageni waliohudhuria sherehe yake walipiga picha na bango hilo.
JE,WEWE UNAIONAJE HII? NI SAHIHI AU KAKOSEA?