Mwili wa Gissima Nyamo-hanga kuzikwa jumatano Aprili 16

Mwili wa Gissima Nyamo-hanga kuzikwa jumatano Aprili 16

#1

Mwili wa Gissima Nyamo-hanga kuzikwa jumatano Aprili 16



Shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco limeeleza kuwa Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la umeme Tanzania Gissima Nyamo-hanga utazikwa nyumbani kwao Migungani, Bunda mkoani Mara Jumatano Aprili 16, 2025.

Kwa mujibu wa shirika la umeme Tanesco kesho Jumanne Aprili 15, 2025 ni maombolezo nyumbani kwa marehemu Oysterbay Jijini Dar Es salaam.

Nyamo-hanga aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo Septemba 23, 2023 akichukua nafasi ya Maharage Chande, kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa wakala wa umeme vijijini Rea.

Kulingana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo, chanzo cha ajali hiyo ni baada ya dereva wa gari hilo aina ya Toyota Landcruiser alilokuwemo Nyamo-hanga, kumkwepa mwendesha baiskeli na kupoteza uelekeo na kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa mbele yao ambapo Nyamo-hanga na dereva wake Muhajir Haule walifariki dunia hapo hapo.

Leo Jumatatu Aprili 14, Shirika la Kenya Power pia limeungana na sekta ya nishati ya Afrika Mashariki kuomboleza kifo cha Eng. Gissima Nyamo-Hanga,wakimtaja marehemu kama kiongozi mwenye maono, ambaye alijitolea kwa dhati kusukuma mbele ajenda ya ushirikiano wa nishati katika ukanda huu.

“Kifo chake ni pigo kubwa kwa sekta ya nishati katika ukanda huu na kimegusa kwa kina TANESCO na uongozi mzima wa Kenya Power,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Katika kipindi kifupi cha uongozi wake, alisukuma mbele ushirikiano muhimu kati ya Kenya na Tanzania katika sekta ya nishati.

“Katika miezi ya hivi karibuni, aliongoza kwa mafanikio timu ya TANESCO katika mazungumzo ya Mkataba wa Kubadilishana Nishati na Kenya Power, jambo lililowezesha uzinduzi na uanzishaji rasmi wa njia ya umeme ya msongo wa kV 400 kati ya Kenya na Tanzania, ambayo sasa inatumika kikamilifu kwa biashara ya umeme mipakani,” ilieleza taarifa ya KPLC.

Kenya Power pia ilimpongeza kwa mchango wake katika Kamati ya Uongozi ya East African Power Pool (EAPP), ambapo alihusika katika kuandaa mazingira ya biashara ya nishati kwa nchi wanachama 13 wa ukanda huu.

“Atakumbukwa kama mjumbe aliyejitolea kwa dhati katika Kamati ya EAPP, akichangia kuweka misingi ya biashara ya umeme ya baadaye katika Afrika Mashariki,”



Reply


image quote pre code