Nini Faida ya kutumia Gari kali Siku ya Harusi?
Bila shaka ushahudhuria vikao vya sherehe mbalimbali iwe sendoff, harusi na nyingine zenye kufanana na hizo, ukaona namna kamati za maandalizi zinavyohaha kuhakikisha maharusi wanatumia magari mazuri siku ya tukio.
Si ajabu ukaona watu wanafikia hata hatua ya kugombana kuhusu gari la maharusi, huyu akisema aina fulani ya gari ndo nzuri lakini gharama kubwa, mwingine akisema tusijali gharama tuichukue tu kama bajeti ipo.
Sasa kuna mdau anasema ushawahi kujiuliza faida ya kutumia gari kali ni ipi? Yaani usiku mtu anatumia gari kali kwenye harusi anapelekwa ukumbini kisha hotelini, halafu asubuhi anaondoka na Bajaji kuelekea nyumbani kwake, mbwembwe zote zimeisha! Je tumsaidie mdau mawazo au asubiri kwenye shughuli yake aone?