RIPOTI MPYA:Vifo wakati wa kujifungua vimepungua kwa asilimia 40%
Wanawake siku hizi wana uwezekano mkubwa kuliko wakati mwingine wowote wa kuishi wakati wa ujauzito na kujifungua, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuhusu hatari ya kurudi nyuma kwa mafanikio haya, huku kukiwa na upungufu wa msaada wa kibinadamu usio na kifani kote duniani.
Ripoti hiyo, “Mwenendo wa vifo wakati wa kujifungua” inaonyesha kuwa kumekuwa na upungufu wa asilimia 40 wa vifo vya kina mama duniani kati ya mwaka 2000 na 2023 mafanikio yaliyotokana zaidi na kuboreshwa kwa upatikanaji wa huduma muhimu za afya.
Hata hivyo, ripoti hiyo inaonyesha kwamba kasi ya maendeleo hayo imepungua sana tangu mwaka 2016, na inakadiriwa kuwa takribani wanawake 260,000 walifariki mwaka 2023 kutokana na matatizo yanayohusiana na ujauzito au kujifungua sawa na kifo kimoja cha mama kila dakika mbili.
Reply
image quote pre code