Connect with us

magonjwa

Sababu za Uric Acid Kuzidi Mwilini,Dalili na Tiba

Doctor Ombeni

Published

on

189 Views
0 Comments

Sababu za Uric Acid Kuzidi Mwilini,Dalili na Tiba

Uric acid ni taka mwili asilia ambayo hutengenezwa wakati mwili wako unapovunja kemikali inayojulikana kama purines, ambayo ni protini zinazopatikana katika vyakula kama vile nyama nyekundu, samaki, na vyakula vingine vya protini. Uric acid kawaida hutolewa kupitia mkojo, lakini inapozidi mwilini, inaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.

Uric acid is a natural waste product formed when your body breaks down chemicals called purine

Sababu za Uric Acid Kuzidi Mwilini:

  1. Kula vyakula vyenye purines nyingi: Vyakula kama vile nyama ya ng’ombe, samaki, na vyakula vya baharini vinavyokuwa na purines nyingi vinaweza kuongeza kiwango cha uric acid mwilini.

  2. Matatizo ya figo: Ikiwa figo Zako hazifanyi kazi ipasavyo, uric acid hushindwa kutolewa vizuri nje ya mwilini wako.

  3. Unywaji wa pombe: Pombe, hasa beer, inaweza kuongeza uzalishaji wa uric acid na kupunguza utoaji wake kutoka mwilini,hali ambayo huweza kupelekea Uric acid kujikusanya zaidi ndani ya mwili.

  4. Uzito mkubwa: Uzito mkubwa,Unene au obesity pia huchangia kuzidi kwa uric acid mwilini kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa asidi hii

  5. Magonjwa mengine: Magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu (high blood pressure), na matatizo ya moyo yanaweza kuchangia ongezeko la uric acid mwilini.

Dalili za Uric Acid Kuzidi:

  1. Gout: Hali ya gout hutokea wakati uric acid inapoelekea kutengeneza vijidudu vya crystals kwenye viungo, hasa kwenye kidole cha mguu, ambayo husababisha maumivu makali, uvimbe, na joto la kiungo kilichoathirika.

  2. Maumivu ya viungo: Uric acid inapozidi, inaweza kuathiri viungo na kusababisha maumivu na uvimbe.

  3. Madhara ya figo: Uric acid inayozidi pia inaweza kuunda mawe kwenye figo (kidney stones), ambayo husababisha maumivu makali wakati wa kukojoa na kuathiri kazi ya figo.

  4. Uchovu na homa: Watu wenye uric acid nyingi mara nyingine wanaweza kuhisi uchovu au kuwa na homa mara kwa mara.

Matibabu ya Uric Acid Kuzidi:

  1. Kula vyakula vyenye afya: Kuepuka vyakula vyenye purines nyingi na kula zaidi matunda, mboga, na nafaka.

  2. Matibabu ya dawa: Zipo Dawa ambazo Zinaweza kutumika kusaidia kupunguza uzalishaji wa uric acid mwilini, wakati dawa nyingine za anti-inflammatory zinaweza kutumika kupunguza maumivu na uvimbe wa gout.

  3. Unywaji wa maji mengi: Kunywa maji ya kutosha husaidia kutoa uric acid mwilini kupitia mkojo.

  4. Kupunguza uzito: Kupunguza uzito na kufanya mazoezi mara kwa mara kunaweza kusaidia kupunguza viwango vya uric acid mwilini.

  5. Kuepuka pombe na sigara: Kuepuka pombe na sigara kunapunguza hatari ya uric acid kuzidi.

Hivyo, ikiwa unashuku kuwa na tatizo la uric acid kuzidi, ni muhimu kufanya uchunguzi,kupata Matibabu, na kufuata Ushauri wa daktari ili kudhibiti hali hii.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

189 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Hospital8 hours ago

MNH-Mloganzila Yafanya Upasuaji wa Kurekebisha na Kurefusha Mifupa kwa Mbinu ya Ilizarov

MNH-Mloganzila Yafanya Upasuaji wa Kurekebisha na Kurefusha Mifupa kwa Mbinu ya Ilizarov Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila imefanikiwa kufanya kwa...

EVENTS10 hours ago

Wavunja Record ya Dunia kwa kupanda miche 2,51,446 kwa saa moja tu

Wavunja Record ya Dunia kwa kupanda miche 2,51,446 kwa saa moja tu. Katika juhudi kubwa za kushangaza kwenye kutunza mazingira,...

magonjwa ya wanawake11 hours ago

Fangasi Ukeni: Chanzo na Dalili

Fangasi Ukeni: Chanzo na Dalili Fangasi ukeni ni maambukizi ya fangasi yanayotokea kwenye uke na mara nyingi husababishwa na fangasi...

magonjwa ya wanawake1 day ago

Hedhi yenye harufu mbaya: SABABU zinazoweza kusababisha

Kwa baadhi ya wanawake, damu ya hedhi inaweza kuwa na harufu fulani ambayo si sawa na harufu ya kawaida ya...

EVENTS1 day ago

Siku ya kuzuia kujiua duniani 2026: kubadili mtazamo na kuanza mazungumzo

SIKU YA KUZUIA KUJIUA DUNIANI 2026: KUBADILI MTAZAMO NA KUANZA MAZUNGUMZO Kaulimbiu ya 2026: “Changing the Narrative on Suicide” –...

Utafiti1 day ago

Vifo Vinavyotokana na Mimba kutunga Nje ya Kizazi

Mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy) ni hali ambayo mimba inajipandikiza nje ya sehemu ya kawaida ya kizazi,Mara nyingi...

Utafiti2 days ago

Ucheleweshaji wa huduma Ndani ya Hospitali Wawa Tishio Kubwa kwa Maisha ya Mama na Mtoto

Ucheleweshaji wa huduma ndani ya vituo vya afya umeonekana kuwa moja ya sababu kubwa zinazochangia vifo vya wajawazito na watoto...

Afya News2 days ago

Jinsi Dawa za Kulevya Zinavyoharibu Afya ya Kinywa na Meno

Matumizi ya dawa za kulevya yanaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili, ikiwemo ubongo, moyo, ini na mfumo wa fahamu. Hata...

magonjwa3 days ago

Ugonjwa wa Selimundu,dalili,chanzo na Tiba

Katika Makala hii tunachambua Zaidi kuhusu Dalili za ugonjwa wa seli mundu,chanzo cha ugonjwa wa Seli mundu pamoja na Matibabu...

Afya News3 days ago

Wataalam wa maabara wahimizwa kuboresha huduma za afya kwa Wananchi

WATAALAM WA MAABARA WAHIMIZWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI Na Zakayo Mosha- WAF Morogoro Wataalam wa Maabara wamehimizwa kutumia...

190
0