Sababu za Uric Acid Kuzidi Mwilini,Dalili na Tiba
Uric acid ni taka mwili asilia ambayo hutengenezwa wakati mwili wako unapovunja kemikali inayojulikana kama purines, ambayo ni protini zinazopatikana katika vyakula kama vile nyama nyekundu, samaki, na vyakula vingine vya protini. Uric acid kawaida hutolewa kupitia mkojo, lakini inapozidi mwilini, inaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.
Uric acid is a natural waste product formed when your body breaks down chemicals called purine
Sababu za Uric Acid Kuzidi Mwilini:
-
Kula vyakula vyenye purines nyingi: Vyakula kama vile nyama ya ng'ombe, samaki, na vyakula vya baharini vinavyokuwa na purines nyingi vinaweza kuongeza kiwango cha uric acid mwilini.
-
Matatizo ya figo: Ikiwa figo Zako hazifanyi kazi ipasavyo, uric acid hushindwa kutolewa vizuri nje ya mwilini wako.
-
Unywaji wa pombe: Pombe, hasa beer, inaweza kuongeza uzalishaji wa uric acid na kupunguza utoaji wake kutoka mwilini,hali ambayo huweza kupelekea Uric acid kujikusanya zaidi ndani ya mwili.
-
Uzito mkubwa: Uzito mkubwa,Unene au obesity pia huchangia kuzidi kwa uric acid mwilini kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa asidi hii
-
Magonjwa mengine: Magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu (high blood pressure), na matatizo ya moyo yanaweza kuchangia ongezeko la uric acid mwilini.
Dalili za Uric Acid Kuzidi:
-
Gout: Hali ya gout hutokea wakati uric acid inapoelekea kutengeneza vijidudu vya crystals kwenye viungo, hasa kwenye kidole cha mguu, ambayo husababisha maumivu makali, uvimbe, na joto la kiungo kilichoathirika.
-
Maumivu ya viungo: Uric acid inapozidi, inaweza kuathiri viungo na kusababisha maumivu na uvimbe.
-
Madhara ya figo: Uric acid inayozidi pia inaweza kuunda mawe kwenye figo (kidney stones), ambayo husababisha maumivu makali wakati wa kukojoa na kuathiri kazi ya figo.
-
Uchovu na homa: Watu wenye uric acid nyingi mara nyingine wanaweza kuhisi uchovu au kuwa na homa mara kwa mara.
Matibabu ya Uric Acid Kuzidi:
-
Kula vyakula vyenye afya: Kuepuka vyakula vyenye purines nyingi na kula zaidi matunda, mboga, na nafaka.
-
Matibabu ya dawa: Zipo Dawa ambazo Zinaweza kutumika kusaidia kupunguza uzalishaji wa uric acid mwilini, wakati dawa nyingine za anti-inflammatory zinaweza kutumika kupunguza maumivu na uvimbe wa gout.
-
Unywaji wa maji mengi: Kunywa maji ya kutosha husaidia kutoa uric acid mwilini kupitia mkojo.
-
Kupunguza uzito: Kupunguza uzito na kufanya mazoezi mara kwa mara kunaweza kusaidia kupunguza viwango vya uric acid mwilini.
-
Kuepuka pombe na sigara: Kuepuka pombe na sigara kunapunguza hatari ya uric acid kuzidi.
Hivyo, ikiwa unashuku kuwa na tatizo la uric acid kuzidi, ni muhimu kufanya uchunguzi,kupata Matibabu, na kufuata Ushauri wa daktari ili kudhibiti hali hii.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code