Serikali yaendelea kutafiti visababishi vya Saratani kanda ya ziwa

Serikali yaendelea kutafiti visababishi vya Saratani kanda ya ziwa

#1

Serikali yaendelea kutafiti visababishi vya Saratani kanda ya ziwa



Serikali imesema inaendelea na utafiti wa kina kubaini visababishi halisi vya saratani katika Kanda ya Ziwa, ambapo aina tano za saratani zimebainika kuongoza katika eneo hilo.

Akijibu swali la Mhe. Kabula Enock Shitobela (Viti Maalum) leo Aprili 14, 2025 Bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema utafiti huo umebaini kuwa saratani zinazoongoza ni za kibofu cha mkojo, mji wa uzazi kwa wanawake, damu, macho na figo.

“Tumechukua sampuli za damu 9,600 kutoka kwa watu wasio na saratani ili kulinganisha na zile za wagonjwa wa saratani. Hii itatusaidia kutambua sababu za msingi za magonjwa haya,” amesema Dkt. Mollel.

Ameongeza kuwa, kwa sasa sababu zinazotajwa kuhusu kuongezeka kwa saratani katika Kanda ya Ziwa bado ni nadharia, na hakuna uthibitisho wa kisayansi hadi utafiti utakapokamilika.

Katika hatua za awali, Serikali kupitia Wizara ya Afya imeelekeza nguvu katika kutoa elimu kuhusu viashiria vinavyohusishwa na saratani, sambamba na utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti Saratani unaojumuisha maeneo saba ya kipaumbele.

Amesema utafiti huo ni sehemu ya juhudi za Serikali kupambana na ongezeko la saratani nchini na kuboresha afya za wananchi hasa katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Reply


image quote pre code