Sokwe Mzee Zaidi Duniani Kusherehekea Miaka 68 Ya Kuzaliwa

Sokwe Mzee Zaidi Duniani Kusherehekea Miaka 68 Ya Kuzaliwa

#1

Sokwe Mzee Zaidi Duniani Kusherehekea Miaka 68 Ya Kuzaliwa



Fatou, ambaye ndiye sokwe mzee zaidi duniani kote anayeishi kwenye uzio, anajitayarisha kutimiza miaka 68.

Wanao mtunza katika bustani ya wanyama ya Berlin siku ya leo  Ijumaa wamkabidhi Fatou kikapu cha matunda na mboga kabla ya siku yake ya kuzaliwa rasmi, ambayo itaadhimishwa siku ya Jumapili.

Fatou alizaliwa mwaka wa 1957 na alipelekwa  kwenye bustani ya wanyama mwaka 1959 katika sehemu ambayo kwa wakati huo ilikuwa Berlin Magharibi. 

Kwa kuwa hana meno tena, watu wanao mtunza wanakikisha kwamba chakula chake ni laini na rahisi kuliwa. Daktari wa mifugo André Schüle amesema kuwa Fatou anapata huduma bora zaidi kwenye bustani hiyo.

Anaishi katika boma lake mwenyewe, mbali na sokwe wengine watano wenye kelele zaidi katika bustani hiyo, ambao wana umri wa kati ya miaka 4 hadi 39.

Fatou alikua mkazi mzee zaidi wa mbuga ya wanyama  mwaka jana, kufuatia kifo cha Ingo flamingo. Ndege huyo aliaminika kuwa na umri wa miaka 75 na alikuwa akiishi kwenye bustani ya wanyama tangu 1955.

WEWE UNA MAONI GANI JUU YA MADA HII,CHANGIA HAPA [REPLY BELOW👇]


image quote pre code