Taifa Stars Yashuka viwango vya soka duniani

Taifa Stars Yashuka viwango vya soka duniani

#1

Taifa Stars Yashuka viwango vya soka duniani



Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetoa viwango vipya vya soka duniani ambapo timu ya Taifa Tanzania Taifa Stars imeshuka kwenye orodha ya kila mwezi ya viwango vya soka duniani inayotolewa na FIFA.

Taifa Stars imeshuka kwa nafasi moja na kufikia nafasi ya 107 kutoka nafasi ya 106 wakati kwa ukanda wa Afrika Mashariki Burundi nayo ikishuka nafasi moja kutoka 139-140 .

Nchi za Afrika Mashariki ni Rwanda ambayo ipo nafasi ya 130, Uganda 89, Kenya 111 huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa nafasi ya 61.

Argentina wameendelea kukamata nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Hispania, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Brazil.

Myanmar ndiyo iliyopanda nafasi nyingi, nafasi saba huku Guinea Bissau ikishuka nafasi nane.

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code