Tanzania yazindua jengo la Mahakama la kwanza kwa ukubwa Afrika na la 6 duniani

Tanzania yazindua jengo la Mahakama la kwanza kwa ukubwa Afrika na la 6 duniani

#1

Tanzania yazindua jengo la Mahakama la kwanza kwa ukubwa Afrika na la 6 duniani



Tanzania imezindua jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama ya nchi hiyo ambalo ni la kwanza kwanza kwa ukubwa barani Afrika na la sita duniani.

Akiongoza shughuli za uzinduzi wa jengo hilo ambalo litatumika kutoa huduma za kimahakama, Rais Samia Suluhu Hassan amesema: ‘’Nimejionea kazi kubwa iliyofanyika, hakika jengo hili lina kila sifa ya kuitwa jengo kuu la mahakama ya Tanzania’’ alisema rais Samia ‘’Baada ya Kazakhstan Tanzania ni ya pili kuwa na chumba cha judiciary’’aliongeza.

Amesema jengo hilo ni urithi wa kipekee unaoleta hadhi, fursa za kiuchumi, na kuvutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi. Amesema hatua hii ni ya kihistoria nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 100 ambayo muhimili wa mahakama haukuwa na ofisi za makao makuu.

Rais Samia ameshukuru mataifa wahisani kwa ufadhili ikiwemo Benki ya dunia kwa kufanikisha ujenzi hu owa jengo la mahakama kuu,Jengo la Tume ya Utumishi wa Mahakama, na majengo ya makazi ya majaji.

Hatua hii sasa inakamilisha mchakato wa dola ya Tanzania kuhamia Dodoma.

Jengo la Mahakama ya Kuala Lumpur, Malaysia ndilo mahakama kubwa zaidi duniani lililojengwa kwa miaka mitatu na kuchukua eneo la hekta 12.

Via BBC

JOIN DISCUSSION [REPLY BELOW]


image quote pre code