TAWA yaua Fisi 43,Oparesheni ya kupambana na Fisi
Katika kupambana na wanyama waharibifu hasa fisi ndani ya Mkoa wa Simiyu Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA), katika Oparesheni yake iliyoanza mwezi Januari, 2025 wamefanikiwa kuua fisi 43.
Hayo yamesemwa Kamanda wa kikosi cha Oparesheni hiyo kutoka TAWA Afisa Mhifadhi daraja la Pili Ayubu Fundi wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo Fisi hao wameuawa katika Wilaya za Itilima, Bariadi pamoja na Maswa.
Amesema kuwa Opareisheni hiyo inatokana na matukio ya Fisi hao kushambulia watu pamoja na mifugo kuongezeka, ambapo Opareisheni imefanyika katika maeneo yote ambayo yameripotiwa uwepo wa wanyama hao.
Naye Afisa Mhifadhi Mwandamizi pamoja na Mahusiano kutoka TAWA Kanda ya Ziwa John Mselikale amewataka wananchi popote ambapo watawaona wanyama hao kutoa taarifa TAWA kwa ajili ya kuwadhibiti.
WEWE UNA MAONI GANI JUU YA MADA HII,CHANGIA HAPA [REPLY BELOW👇]
image quote pre code