Tetemeko la Ardhi laua Watu zaidi ya 1,700 nchini Myanmar

Tetemeko la Ardhi laua Watu zaidi ya 1,700 nchini Myanmar

#1

Tetemeko la Ardhi laua Watu zaidi ya 1,700 nchini Myanmar



Watu zaidi ya 1,700 wamepoteza maisha, kufikia siku ya Jumamosi nchini Myanmar kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lilitokea katika maeneo mengi ya nchi na hata kuathiri mataifa jirani ambapo watu tisa wameuawa nchini Thailand na wajenzi karibu 100 hawajapatikana.

Inahofiwa kuwa idadi ya maafa itaongezeka wakati huu, maafisa wa uokoaji wanapoendelea na jitihada za uokozi, kuwatafuta mamia ya watu ambao hawajapatikana.



Tetemeko hilo la ardhi liliharibu majengo, na barabara katika majimbo mbalimbali huku uogozi wa kijeshi akiomba msaada wa nchi mbalimbali kuwasaidia watu wake.

China, Marekani, India na Korea Kusini ni miongoni mwa nchi ambazo zimeanza kutuma misaada kama vyakula, dawa na hata fedha kuisadia Mynmar kipindi hiki kigumu.

Nchini Thailand, watalaam wa uokoaji wamesema wanawatafuta watu waliokwamama kwenye jengo la ghorofa lililiporomoka jijini Bangkok, baada ya kubainika kuwa bado wako hai.

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code