Ugonjwa wa Chagas ni nini? Chanzo na Tiba yake
Kulingana na Shirika la Afya Duniani WHO mwaka huu, kaulimbiu ni “Kuzuia, Kudhibiti na Kutoa Huduma: Kila Mtu Ana Wajibu Katika Kukabiliana na Ugonjwa wa Chagas.”Duniani kote, watu zaidi ya milioni 100 wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huu, huku takriban watu milioni 7 wakiishi tayari na ugonjwa huo.
Ugonjwa wa Chagas ni nini?
Ugonjwa wa Chagas ni maradhi yanayoweza kuhatarisha maisha, yanayosababishwa na vijidudu au parasite aina ya Trypanosoma cruzi. Kwa mujibu wa WHO kwa kawaida, ugonjwa huu hupatikana zaidi katika Ukanda wa Amerika Kusini, lakini kutokana na safari na uhamiaji wa Watu, visa vya ugonjwa huu vimeripotiwa pia katika maeneo mengine duniani.
🦟 Husambazwa vipi?
Ugonjwa huu huenea zaidi kupitia kung’atwa na mdudu anayejulikana kama “kissing bug” kwa sababu hupenda kung’ata sehemu za uso kama vile mdomo au macho wakati mtu amelala.
Pia unaweza kuambukizwa kupitia:
- Kuchangia damu
- Upandikizaji wa viungo vya mwili
- Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito
- Kula chakula kilicho na vimelea n.k.
🩺 Dalili zake ni zipi?
Ugonjwa wa Chagas una hatua mbili:
Hatua ya awali: wiki au miezi michache baada ya maambukizi
Mara nyingi hakuna dalili au dalili huwa hafifu;
Wengine hupata homa, uchovu, macho kuvimba, maumivu ya mwili, upele n.k.
Watu wengi huwa hawajui kama wameambukizwa
Hatua ya muda mrefu: miaka baadaye endapo haitatibiwa
Huathiri moyo, mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, na mfumo wa neva
Takribani asilimia 30 ya wagonjwa hupata matatizo ya moyo, na asilimia 10 matatizo ya tumbo au neva
💊 Je, unatibika?
✅ Ndiyo- ukiugundua mapema, ugonjwa huu unatibika kwa kutumia dawa za kuua vimelea kama benznidazole au nifurtimox.
Katika hatua ya muda mrefu, matibabu husaidia kudhibiti dalili na kupunguza kasi ya madhara makubwa.
📌 Kwa nini ugonjwa huu ni hatari?
Ingawa unaathiri mamilioni ya watu hasa katika maeneo ya vijijini na maskini mara nyingi hupuuzwa kwa sababu dalili zake huwa za taratibu na zinaweza kujificha kwa miaka mingi.
Ndiyo maana mashirika kama WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF yanafanya kampeni ya kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huu kila mwaka Aprili 14 katika Siku ya Kimataifa ya Ugonjwa wa Chagas.
Je,Una tatizo Lolote,Usisite tuwasiliane kupitia namba Zetu za Kila Siku!
Reply
image quote pre code