Ushuru Mpya watangazwa na Trump,Waacha Dunia Midomo wazi
Baada ya miezi miwili ya maandalizi, Rais wa Marekani Donald Trump ameanzisha vita vipya vya kibiashara, akitangaza hatua kali za ushuru dhidi ya bidhaa zinazoingia nchini humo.
Katika hafla iliyofanyika katika bustani ya Ikulu ya White House, Trump alitangaza Aprili 2 kuwa “Siku ya Ukombozi” wa kiuchumi kwa Marekani. Akisisitiza kuwa hatua hizi zitawalazimisha washirika wa kibiashara kufanya makubaliano yenye manufaa kwa taifa lake, Trump alisema:
“Tutaifanya Marekani kuwa kubwa na tajiri tena. Nchi yetu imenyang’anywa kwa zaidi ya miaka 50, lakini hilo halitafanyika tena.”
Kupitia amri ya kiutendaji, Trump ameweka ushuru wa kulipiza kisasi wa:
34% dhidi ya Uchina
20% dhidi ya Jumuiya ya Ulaya
24% dhidi ya Japan
26% dhidi ya India
Kwa mataifa masikini kama Vietnam na Myanmar, ushuru umeongezeka hadi 50%, huku kiwango cha chini kwa bidhaa zote kutoka nje kikiwa 10%. Ushuru huu utaanza kutumika Aprili 5, huku viwango vya juu zaidi vikianza Aprili 9.
Wanauchumi wameonya kuwa hatua hizi zitafanya maisha kuwa magumu kwa wote, ikiwa ni pamoja na Wamarekani, ambao sasa watalazimika kulipa gharama kubwa zaidi kwa bidhaa za nje.
Hata hivyo, Trump amesema yuko tayari kwa mazungumzo na kwamba mataifa yanayopinga ushuru huu yana fursa ya kuondoa ushuru wao dhidi ya Marekani ili kuepuka athari zaidi.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code