Usonji huathiri takriban mtoto 1 kati ya 100 ulimwenguni kote

Usonji huathiri takriban mtoto 1 kati ya 100 ulimwenguni kote

#1

Usonji huathiri takriban mtoto 1 kati ya 100 ulimwenguni kote



Ni vigumu kuwatambua na kuwatofautisha kwa kuwatazama watoto wenye Usonji, huu ni muda wa mapumziko na wanafunzi wengi wanaofundishwa katika kituo hiki maalumu cha watoto wenye ulemavu, wanacheza michezo mbali mbali wakiwa nje ya madarasa yao.

Mwalimu wa wanafunzi wenye ulemavu Catherine Akyoo kutoka kituo hiki maalumu kilichopo USA River jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania, anasema sio kazi rahisi kuwafundisha lakini wanaelewa taratibu na elimu wanayoipata shuleni hapo, inawasaidia kupata ujuzi wa shughuli za mikono na kujiajiri.

Usonji ama Autism kwa kingereza, ni tatizo la kibaiolojia analopata mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake na dalili huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea.

Umuhimu wa huduma na msaada unaopatikana

Wataalamu wa afya wanasema sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuzitanmbua dalili hizo, lakini  miongoni mwa dalili ni mtoto kushindwa kuzungumza na wakati mwingine anajing'ata.

Shirika la afya ulimwenguni linasema watoto wengi wenye tatizo hilo hutelekezwa na jamii na kunyimwa haki zao za msingi ikiwapo kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa. Lakini jamii inapaswa ipewe elimu ya jinsi ya kuwasaidia watoto wenye Usonji. 

Nchini Tanzania harakati za kuelimisha jamii kuhusu Usonji zinafanyika katika maeneo mbali mbali, japo tatizo hilo halijatambulika vizuri kwenye jamii.

Takiwmu kuhusu Usonji

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la afya Duniani WHO, Usonji huathiri takriban mtoto 1 kati ya 100 ulimwenguni kote. Ingawa dalili za Usonji zinaweza kuonekana mapema utotoni, mara nyingi utambuzi hufanyika baadaye.

Shirika la WHO linasema ugunduzi wa mapema na uingiliaji kati unaweza kuboresha mawasiliano na mnepo wa kijamii dhidi ya ugonjwa huo, na hivyo kuimarisha ustawi wa watu wenye Usonji pamoja na walezi wao.

#SOMA hapa; Kuhusu Tatizo la Usonji,Chanzo,Dalili na Tiba

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code