Utaweza Kuishi Marekani Ukitoa Billion 13 Tsh,Trump aja na hii

Utaweza Kuishi Marekani Ukitoa Billion 13 Tsh,Trump aja na hii

#1

Utaweza Kuishi Marekani Ukitoa Billion 13 Tsh,Trump aja na hii



Rais wa Marekani Donald Trump ameitangaza na kuionesha rasmi kadi ya gold (Gold Card au Trump Card) yenye sura ya Trump ambayo itagharimu USD milioni 5 (Tsh. bilioni 13.375) ambapo Mtu atakayenunua atapata fursa ya kuwa na makazi ya kudumu nchini Marekani kama ilivyo kwa Watu wenye green card.

Mpango wa kuanzishwa kwa kadi hizo ulitangazwa kwa mara ya kwanza na utawala wa Trump mwezi February mwaka huu ambapo Trump amesema ndani ya Wiki mbili kutoka sasa kadi hizo zitaanza kuuzwa zikiwalenga zaidi Raia wa kigeni wenye uwezo mkubwa wa kiuchumi ambapo Trump analenga kuongeza kipato kwa Taifa la Marekani kupitia kadi hizo na tayari Trump amesema kadi ya kwanza ameinunua yeye mwenyewe.

Miongoni mwa faida za kadi hizo ni kupata haki ya makazi ya kudumu nchini Marekani, kupata uwezekano rahisi zaidi wa kupata Uraia wa Marekani, itazisaidia kampuni za Marekani kuwaingiza Wafanyakazi wenye uwezo mkubwa wa kazi nchini humo ili wasaidie kuongeza uchumi, pia ni njia rahisi zaidi ukilinganisha na mfumo wa kupata greed card ambazo mchakato wake una vipengele vingi na hata wengine kutapeliwa wakati wakipambania uraia wa Marekani.

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code