Wakili Pheroze Nowrojee wa nchini Kenya afariki dunia
Wakili Mkongwe Pheroze Nowrojee amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria nchini Kenya Faith Odhiambo amethibitisha.
Odhiambo alimsifu Nowrojee kama mtu mwenye utulivu na tabia ya heshima, ambaye maisha yake yalidhihirisha wajibu wa kutumikia na kujitolea kwenye masuala ya haki.
"Ni siku ya huzuni kwa taaluma ya sheria tunapomuaga mtu ambaye alitufundisha maana ya kuwa wataalamu mashuhuri.
Mioyo yetu inazizima leo, kwani tumempoteza mmoja wa watu wakuu zaidi kuwahi kufanya hivyo," alisema.
"Tunapoenzi kiongozi huyu katika kuheshimu katiba, tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia yake, marafiki, na kila mtu ambaye ameguswa na maisha yake.
''Wakili Pheroze Nowrojee apumzike kwa amani ya milele." Faith Odhiambo alieleza