Watalii walio katika hedhi wazuiwa kuingia kwenye Mahekalu

Watalii walio katika hedhi wazuiwa kuingia kwenye Mahekalu

#1

Watalii walio katika hedhi wazuiwa kuingia kwenye Mahekalu


Mamlaka huko Bali, Indonesia imezindua sera mpya ya kupiga marufuku "watalii walio katika hedhi" kuingia mahekaluni kwa wasiwasi kwamba damu ya kipindi cha Hedhi ni "chafu" itachafua maeneo yao matakatifu.

Sheria hii "Unorthodox law" imejumuishwa katika orodha ya sera ambazo gavana wa kisiwa cha tropiki, Wayan Koster, aliziweka mnamo Machi 24 ili kuwabana "watalii wanaoenda kinyume",Hii ni kulingana na ripoti kutoka Metro.

 "Ninatekeleza waraka huu kama hatua ya haraka ya kudhibiti watalii wa kigeni wanapokuwa Bali," honcho ilitangaza.

Chini ya sheria hizo mpya, wanawake hawataruhusiwa kuingia kwenye mahekalu ya Balinese wakiwa kwenye hedhi kwa kuhofia kwamba Damu ya hedhi ni "chafu" na "itafanya hekalu kuwa najisi," Visit Bali iliripoti.

Kulingana na Stories zilizokuwa zinasimuliwa kutoka "kizazi hadi kizazi, kuna athari mbaya ikiwa umeamua kuingia hekaluni wakati wa hedhi," tovuti hiyo ilionya.

"Wanawake wengi hupata maumivu na kuzimia wakiwa hekaluni. Na Inaripotiwa kwamba kuna matukio mengine mengi ya ajabu ambayo yanaweza kuwapata wanawake walio kwenye hedhi wakiwa kwenye mahekalu hayo."

Na sio tu wanawake wenye hedhi walioathiriwa, kulingana na tovuti hiyo ilitangaza kwamba "wakazi karibu na hekalu wanaweza kuathiriwa na majanga ya asili na magonjwa" yaliyosababishwa na wanawake kuingia hekaluni wakiwa kwenye kipindi cha Hedhi.

TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code