Watu wapatao 45 wamepoteza maisha chanzo Imani za Kishirikina

Watu wapatao 45 wamepoteza maisha chanzo Imani za Kishirikina

#1

Watu wapatao 45 wamepoteza maisha chanzo Imani za Kishirikina.



Kwa Mujibu wa taarifa kutoka Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma kitengo cha Kamisheni ya Polisi Jamii Dawati la ushirikishwaji Tanzania zinaeleza Watu wapatao 45 wamepoteza maisha yao huku chanzo kikidaiwa kuhusishwa na Imani za Kishirikina.

Hayo yameelezwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma kitengo cha Kamisheni ya Polisi Jamii Elisante Ulomi wakati alipokuwa akitoa Mafunzo na Elimu kwa Polisi Jamii pamoja na Makampuni ya Ulinzi Mjini Geita lengo likiwa ni kudhibiti Uharifu kwenye Maeneo ambapo Mafunzo hayo yameratibiwa na Mgodi wa Dhahabu GGML kwa kipindi cha siku 14. 

“ Takwimu za toka Mwaka 2021 hadi 2024 zinaonyesha kwamba takribani Watu 45 wamepoteza maisha yao kwa ajili ya vyanzo vile vya vifo vyao vikiwa vinaonekana kwamba vimetokana na imani au mauwaji hayo yametokana na Imani Potofu za ushirikina“ Kamishina Msaidizi wa Polisi Makao Makuu Dodoma , Elisante Ulomi. 

Aidha Ulomi amesema imani za kishirikina zimekuwa zikichochewa na Umasikini pamoja na elimu ambapo amesema elimu waliyoitoa itakwenda kuisaidia Jamii kuepukana na Madhira hayo ambayo wao wamekuwa mstari wa Mbele kupinga mauwaji ambayo yamekuwa yakisababishwa na imani za kishirikina.

JOIN DISCUSSION [REPLY BELOW]


image quote pre code