WHO: Kifua Kikuu kinaua karibu watu mil 1.5 kwa mwaka
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani Shirika (WHO), kupungua kwa kasi kwa ufadhili wa misaada ya maendeleo kunatishia mafanikio katika vita dhidi ya ugonjwa hatari zaidi wa Kifua Kikuu (TB).
Katika ripoti ya WHO iliyotolewa siku ya Jumatatu, shirika hilo la afya lilisema kuwa TB bado inaua takriban watu milioni 1.5 kila mwaka.
Watu milioni 79 wameokolewa kupitia utambuzi wa mapema na matibabu tangu mwaka wa 2000. Lakini bila ufadhili zaidi, hali inaonekana kuwa mbaya kwa nchi maskini zaidi, ilisema WHO katika ripoti yake iliyochapishwa siku ya Kifua Kikuu Duniani ambayo haudhimishwa tarehe 24 mwezi Machi kila mwaka.
Marekani imezuia mabilioni ya dola katika misaada mbalimbali ya kifedha. Lakini nchi zingine, kama vile Uingereza mnamo mwaka 2025 na Ujerumani mwaka 2024, pia zilitangaza kupunguzwa kwa misaada ya maendeleo.
WHO inaripoti kuwa mipango ya kupambana na TB iko katika hatari ya kuporomoka katika nchi 27. Ripoti hiyo inaeleza kwamba bila ufadhili kutoka nje ya nchi, watu wachache wataweza kufanya vipimo, visa vichache kutambuliwa na kutibiwa pamoja na ufuatiliaji kidogo. Matokeo yake, inasema ripoti hiyo watu wengi wataambuizwa.
Nchi tisa tayari zina matatizo ya kupata dawa. Mapema 2023, ni robo tu ya ufadhili wa dola bilioni 22 unaohitajika kupambana na TB uliweza kupatikana, kulingana na WHO.
Visa vya TB miongoni mwa watoto vyaongezeka Ulaya na Asia ya Kati
Watoto walio chini ya umri wa miaka 15 walichangia asilimia 4.3 ya wagonjwa wapya na wanaougua tena ugonjwa wa kifua kikuu katika kanda ya Ulaya mwaka 2023, ikiwa ni nyongeza ya asilimia 10 zaidi ya miezi 12 iliyopita.Bado kuna changamoto ya kuudhibiti Ugonjwa wa kifua kikuu
Zaidi ya watu 172,000 kwa ujumla wameripotiwa kuwa na visa vipya vya ugonjwa huo katika nchi 53, pamoja na kadhaa za Asia ya kati.
Matokeo ya ripoti hiyo yanaonyesha kwamba kuenea kwa TB "bado kunaendelea" katika kanda hizo, huku mashirika ya afya yakibainisha kuwa "hatua za haraka za afya ya umma zinahitajika kudhibiti na kupunguza mzigo unaokua wa TB".
Maambukizi na dalili
Karibu robo ya watu duniani tayari wameambukizwa bakteria wa TB. Hata hivyo, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, ni kati ya asilimia 5 hadi 10 tu ya waliombukizwa wanaopata dalili na kuugua TB kamili.
Dalili za kifua kikuu zinaweza kuwa kama ifuatavyo. Kikohozi kinachodumu kwa muda mrefu, wakati mwingine chenye damu, maumivu ya kifua, udhaifu wa mwili na uchovu wa mara kwa mara, kupungua uzito bila sababu, homa, kutokwa na jasho jingi usiku.
TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)
image quote pre code