WHO:Takribani wanawake 300,000 wanaendelea kufariki dunia kila mwaka wakati wa ujauzito au kujifungua

WHO:Takribani wanawake 300,000 wanaendelea kufariki dunia kila mwaka wakati wa ujauzito au kujifungua

#1

WHO:Takribani wanawake 300,000 wanaendelea kufariki dunia kila mwaka wakati wa ujauzito au kujifungua 




Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO ambalo linaanzisha kampeni ya mwaka mzima kuhusu afya ya mama na mtoto mchanga “Takribani wanawake 300,000 wanaendelea kufariki dunia kila mwaka wakati wa ujauzito au kujifungua na zaidi ya watoto milioni mbili hufariki dunia ndani ya mwezi wao wa kwanza wa maisha huku wengine takribani milioni mbili huzaliwa wakiwa tayari wamekufa.”

Takwimu hizi zinaonyesha kuwa kuna kifo kimoja kinachozuilika kila sekunde saba, limesema shirika hilo la afya Duniani.

Kampeni hiyo ya WHO "Mwanzo wenye afya, mustakabali wenye matumaini" inazitaka serikali na watunga sera za afya kuongeza juhudi za kumaliza vifo vya kina mama na watoto wachanga vinavyoweza kuzuilika, na kuweka kipaumbele kwa afya na ustawi wa wanawake kwa muda mrefu.

Kumsaidia kila mama na mtoto kuishi na kustawi
Kupitia hatua za kimkakati, WHO inalenga si tu kuokoa maisha, bali kuhakikisha kuwa kinamama na watoto wanastawi.

Kwa kushirikiana na wadau, WHO itajikita katika kuwawezesha wataalamu wa afya na kusambaza taarifa muhimu kuhusu ujauzito wenye afya, kujifungua salama, na huduma ya baada ya kujifungua.

Kuwasikiliza wanawake
Upatikanaji wa huduma za afya za hali ya juu na zenye kujali ni jambo la msingi kwa wanawake na familia zao kila mahali, linasisitiza Shirika la WHO.

Limeongeza kuwa mifumo ya afya lazima ibadilike ili kushughulikia masuala mbalimbali ya kiafya, yakiwemo matatizo ya uzazi, changamoto za afya ya akili, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, na upangaji uzazi kuhakikisha kwamba mahitaji ya wanawake yanatimizwa kabla, wakati na baada ya kujifungua.

JOIN DISCUSSION [REPLY BELOW]


image quote pre code