Wizara ya Afya yaingilia kati Sakata la Mama kubadilishiwa mtoto baada ya kujifungua

Wizara ya Afya yaingilia kati Sakata la Mama kubadilishiwa mtoto baada ya kujifungua

#1

Wizara ya Afya yatoa Ufafanuzi kuhusu Sakata la Mama kubadilishiwa mtoto baada ya kujifungua



Wizara ya Afya imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa inayosambaa mitandaoni inayodai kuwa Neema Kilugala, mkazi wa Daraja Mbili mkoani Arusha, alibadilishiwa mtoto baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, mnamo Machi 24, 2025.

Kwa mujibu wa Neema, baada ya kujifungua, alioneshwa mtoto wake akiwa mzima na muuguzi aliyemhudumia. Hata hivyo, alipomletewa mtoto wake baadaye, alibaini kuwa alikuwa amefungwa vitenge visivyo vyake, hali iliyozua wasiwasi.

Muuguzi aliyekuwa akihudumu hospitalini hapo alidai kuwa kulikuwa na mkanganyiko wa vitenge, na kwa kutambua hali hiyo, alijaribu kurekebisha tatizo hilo. Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha na Jeshi la Polisi, imechukua hatua za haraka kuchunguza suala hilo, ikiwemo:

(1) Kuchukua sampuli za vinasaba (DNA) kwa wazazi waliojifungua wakati huo pamoja na za watoto wao ili kubaini ukweli katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

(2) Kumsimamisha kazi muuguzi husika ili kupisha uchunguzi.

Wizara ya Afya imesisitiza kuwa uchunguzi wa kina utafanyika, na mara utakapokamilika, taarifa rasmi itatolewa na hatua stahiki kuchukuliwa.



TOA MAONI YAKO HAPA(REPLY BELOW👇)


image quote pre code