Connect with us

magonjwa

Maumivu wakati wa kukojoa kwa Mwanamke na Mwanaume

Doctor Ombeni

Published

on

Maumivu wakati wa kukojoa (Dysuria) ni hali ya kuhisi kuungua, kuchoma au maumivu wakati wa kutoa mkojo. Hali hii inaweza kumpata mwanamke au mwanaume, na chanzo kinaweza kutofautiana kutegemea jinsia na hali ya kiafya. Hapa chini ni sababu kuu kwa kila jinsia:

SABABU ZA MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA KWA MWANAMKE

1. Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI)

Hii ndiyo sababu kuu kwa wanawake.

Bakteria huingia kwenye urethra na kusababisha maambukizi.

Dalili kuu ikiwemo: Maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, harufu mbaya ya mkojo, mkojo kuwa na rangi isiyokawaida,maumivu ya viungo,homa n.k.

2. Maambukizi ya ukeni ambayo

Husababishwa na fangasi (candida), bakteria, au Trichomoniasis.

Hali hii Inaweza kuathiri uke na kusababisha maumivu wakati wa kukojoa au tendo la ndoa.

Yapo Maambukizi ya zinaa (STIs)

  • Kama vile Chlamydia, Gonorrhea, Herpes au Trichomoniasis.
  • Maambukizi haya huweza kuambatana na dalili kama vile uchafu ukeni, maumivu chini ya tumbo, maumivu wakati wa kukojoa na kuwashwa sehemu za Siri.

3. Matumizi ya sabuni au kemikali kali Ukeni

Baadhi ya Sabuni za kuosha uke, poda, au dawa za kupunguza harufu zinaweza kusababisha mabadiliko makubwa ya hali asilia ya ukeni kutokana na kemikali kali au viambato flani ndani yake,hali ambayo huweza kupelekea hatari ya mashambulizi zaidi ya fangasi au bacteria na kuleta dalili kama vile kuwasha na maumivu wakati wa kukojoa au tendo la ndoa.

4. Matatizo ya kibofu cha mkojo

Pia Kuvimba au kuambukizwa kwa kibofu cha mkojo kunaweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa.

SABABU ZA MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA KWA MWANAUME

1. Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)

Hali hii pia huweza kuwa miongoni mwa Sababu kubwa sana za maumivu wakati wa kukojoa,kuhisi hali ya kuungua au kuwaka moto wakati wa kukojoa kwa Mwanaume.

2. Maambukizi au magonjwa ya zinaa (STIs)

Magonjwa ya Zinaa kama vile;

  • Chlamydia, Gonorrhea, Herpes ni sababu kubwa pia ya maumivu kwa wanaume.

Dalili zinaweza kujumuisha usaha kutoka kwenye uume, kuwasha, na maumivu wakati wa kukojoa.

3. Ugonjwa wa Tezi Dume au (kuvimba kwa tezi dume – Prostate)

Hali hii Huathiri wanaume hasa wenye umri wa kati au wazee.

Dalili huweza kuwa: Maumivu wakati wa kukojoa, maumivu ya nyonga, Sehemu ya chini ya tumbo, na kujisikia hali ya kubanwa mkojo mara kwa mara.

4. Kuvimba kwa korodani au epididymis (orchitis/epididymitis)

Ingawa maumivu ni kwenye korodani, yanaweza kusambaa hadi urethra na kuleta maumivu wakati wa kukojoa.

5. Kuwepo kwa mawe kwenye kibofu au figo

Mawe yanaweza kukwaruza njia ya mkojo na kusababisha maumivu makali wakati wa kutoa mkojo.

SABABU ZINGINE ZA JUMLA ZINAZOWEZA KUTOKEA KWA WOTE (MWANAMKE & MWANAUME)

  • Kunywa maji kidogo,hii hukuweka kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa kama UTI
  • kuwa na Vidonda ndani ya urethra au kibofu
  • Tatizo la Saratani ya kibofu au urethra (ingawa ni nadra lakini inawezekana pia)

Je,Unatatizo hili na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti1 day ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka Vinavyosababishwa na Magonjwa ya Moyo na Kiharusi – Utafiti...

Afya News1 day ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo vitatu vyaripotiwa wiki hii Mtoto mchanga nchini Marekani amefariki dunia...

CHANJO1 day ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola zinatarajiwa kuongezwa kwenye...

Afya News2 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke. Bodi ya Dawa na Sumu...

magonjwa2 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA NINI? Mikono kufa ganzi ni hali ambayo mtu hupoteza hisia...

Uzazi&Ujauzito3 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti5 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...

afyatips5 days ago

Upungufu wa Vitamini D,Dalili Zake, Visababishi na Madhara Ambayo Unaweza Usiyatambue Mapema

Patient Story Via BBC;Sikujua nilikuwa na upungufu wa vitamini D hadi nilipozirai kazini’ Msichana mwenye umri wa miaka 23, Saskia...