Connect with us

Afya News

Siku ya Uchangiaji damu duniani,Hospital ya Muhimbili pekee inahitaji zaidi ya chupa 150 za damu kwa siku

Doctor Ombeni

Published

on

Imeboreshwa August 2, 2026 by Doctor Ombeni

Siku ya Uchangiaji damu duniani,Hospital ya Muhimbili pekee inahitaji zaidi ya chupa 150 za damu kwa siku

Kila siku Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), inahitaji zaidi ya chupa 150 za damu, ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji, wanaojifungua, watoto wachanga na waathiriwa wa ajali.

Mhamasishaji wa Uchangiaji Damu kutoka MNH, Richard Msam, amesema hayo,huku wafanyakazi wa kampuni ya Kefa wakichangia chupa 31.

Amesema malengo ya maadhimisho hayo ni kuokoa maisha ya maelfu ya wagonjwa wanaohitaji damu kwa dharura katika hospitali hiyo, kila siku.

“Mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kila siku. Kwa siku tunahitaji zaidi ya chupa 150 za damu, ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji, akinamama wanaojifungua, watoto wachanga na wahanga wa ajali mbalimbali,” amesema Msam.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano kampuni hiyo, Deogratius Chacha, amesema kampuni imetambua umuhimu wa damu salama katika kuokoa maisha na hivyo kuamua kushiriki kikamilifu katika kuchangia damu.

“Tunatambua kuwa damu haiwezi kutengenezwa viwandani, bali hutolewa na binadamu kwa hiari. Kwa sababu hiyo, tumepata fursa ya kutoa mchango wetu katika kuokoa maisha. Tunatoa wito kwa jamii nzima kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara,” amesema.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu Duniani, ni ‘Changia Damu, Leta Matumaini pamoja, Okoa Maisha’, ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kushiriki kwa hiari katika zoezi la uchangiaji damu.

🏆Certified| Doctor from Afyaclass.Hapa utapata Ushauri & Tiba juu ya magonjwa mbali mbali. Kwa msaada Zaidi Tuwasiliane kupitia namba: +255758286584.Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *