Connect with us

Afya News

Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kuongezeka

Doctor Ombeni

Published

on

Hatua ya Marekani kusitisha msaada wa kigeni umeathiri pakubwa mpango wa utafiti wa chanjo ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) nchini Afrika Kusini, hatua yenye athari kubwa kote duniani na hususan barani Afrika.

Ilikuwa imesalia wiki moja tu kabla ya wanasayansi wa Afrika Kusini kuanza majaribio ya kimatibabu ya chanjo ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), na matumaini yalikuwa makubwa ili kufikia hatua nyingine ya kujaribu kukabiliana na moja ya magonjwa hatari zaidi katika historia.

Na ndipo barua pepe iliwasili ikiwaamuru wanasayansi hao kusitisha shughuli zote. Marekani chini ya utawala wa rais Donald Trump ulikuwa umesitisha ufadhili wake wote katika mradi huo wa majaribio. Taarifa hizo ziliwakwaza mno watafiti, wanaoishi na kufanya kazi katika eneo ambalo  watu wengi wanaishi na VVU  kuliko mahali pengine popote duniani.

Mradi huo wa utafiti unaoitwa BRILLIANT, ulikusudiwa kuwa wa hivi punde zaidi unaotumia mchanganyiko wa tofauti za vijinasaba na utaalamu wa kina wa eneo hilo ili kuwanufaisha waathirika wa virusi vya Ukimwi kote duniani.

Lakini dola milioni 46 kutoka Marekani zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya mradi huo zilitoweka, kufuatia kusitishwa kwa misaada ya kigeni na mfadhili mkuu duniani mapema mwaka huu, hasa kutokana na hatua ya Rais Donald Trump kutangaza kuwa kwa sasa anazingatia kwanza vipaumbele vya taifa lake.

Afrika Kusini yaathirika mno na hatua hiyo

Afrika Kusini imeathirika kwa kiasi kikubwa na hatua hiyo hasa baada ya Trump kutoa madai yasiyokuwa na msingi kwamba utawala umekuwa ukiwalenga jamii ya walio wachache wa Afrika Kusini, wazungu. Nchi hiyo imekuwa ikipokea takriban dola milioni 400 kwa mwaka kupitia mashirika ya misaada ya USAID na PEPFAR yanayolenga kukabiliana na VVU. Lakini sasa misaada yote hiyo imetoweka.

Glenda Grey, ambaye anaongoza mradi huo wa Brilliant, amesema bara la Afrika limekuwa na jukumu muhimu katika kufikia mafanikio ya  dawa za VVU , lakini kusitishwa kwa msaada wa Marekani kunatishia uwezo wa bara hilo kuendelea na jukumu hilo katika siku zijazo.

Maendeleo makubwa yaliyoshuhudiwa ni pamoja na majaribio ya kimatibabu ya dawa aina ya “lenacapavir”, chanjo pekee duniani ya kuzuia kuenea kwa VVU ambayo muathirika huchomwa mara mbili kwa mwaka. Chanjo hiyo iliidhinishwa kwa matumizi rasmi hivi majuzi na mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani (FDA),  na utafiti wake uliwahusisha vijana wa Afrika Kusini.

“Tunafanya majaribio vizuri zaidi, kwa haraka na kwa bei nafuu kuliko mahali pengine popote duniani, na hivyo bila Afrika Kusini kuwa sehemu ya programu kama hizi, bila shaka dunia itaathirika zaidi.” Grey alisema akisisitiza kuwa hayo ni maoni yake. Alibainisha kuwa wakati wa janga la UVIKO-19, Afrika Kusini ilichukua jukumu muhimu kwa kuzijaribu chanjo za Johnson & Johnson na Novavax, uchunguzi uliopelekea wanasayansi wa  Afrika Kusini  kugundua aina nyingine ya virusi hivyo.

Grey anasikitika kushuhudia katika taifa ambalo karibu asilimia 46 ya vijana hawana ajira, maabara zikiwa tupu huku maelfu ya wanasayansi wakiachishwa kazi ikiwa ni pamoja na timu ya watafiti wa Chuo Kikuu cha Witwatersrand iliyokuwa sehemu ya kitengo kinashiriki mpango wa majaribio wa kutengeneza chanjo hiyo ya kuzuia VVU. Ameongeza pia kuwa hatua hiyo inawanyima fursa ya kushirikiana na wanasayansi wengine wa Afrika.

Profesa Abdullah Ely aliyekuwa akiongoza timu hiyo ya watafiti amesema kazi waliyokuwa wakiifanya ilikuwa imeanza kuonyesha matokeo chanya yanayodhihirisha kuwa chanjo hizo zilikuwa na uwezo wa kutoa kinga, lakini akasikitika kuona kwamba juhudi zote hizo sasa zimelazimika kusitishwa.

BRILLIANT sasa inahangaika kutafuta fedha za kuokoa mradi huo .Ununuzi wa vifaa muhimu umesimama na idara ya afya ya Afrika Kusini inasema watafiti wapatao 100 wa mradi huo na wengine wanaohusishwa na miradi ya VVU wameachishwa kazi. Ufadhili wa mpango wa kuwahusisha wanafunzi wanaosomea udaktari katika majaribio ya miradi hiyo uko pia hatarini.

Serikali ya Afrika Kusini inakadiria kuwa miradi ya wanasayansi kuhusu magonjwa ya VVU  na hata kifua kikuu itapoteza karibu dola milioni 107 kutokana na hatua ya Marekani kusitisha misaada ya kigeni, huku ikisisitiza kuwa itakuwa vigumu kupata fedha zitakazoweza kuziba pengo la ufadhili wa Marekani.

Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kuongezeka

Hatua hiyo itapelekea pia dawa za kupunguza makali ya VVU kuwa vigumu kupatikana. Angalau maafisa wa afya 8,000 nchini Afrika Kusini waliokuwa wakifanya kazi katika mpango wa VVU tayari wamefutwa kazi, kulingana na serikali. Pia, timu ya wauguzi waliokuwa wakikusanya data na kufuatilia hali jumla ya wagonjwa ikiwa ni  pamoja na washauri wa ugonjwa wa VVU ambao wangeliweza kuwafikia wagonjwa walio katika mazingira magumu ya vijijini pia wametoweka.

Katika ziara yake nchini Afrika Kusini mwezi Juni, mkurugenzi mtendaji wa shirika la kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa,  UNAIDS Winnie Byanyima alitambua kuhusu dharura iliyopo na maisha ya mamilioni ya watu yaliyokuwa hatarini kutokana na hatua hiyo hasa ikizingatiwa kuwa miradi ya utafiti na huduma za afya nchini Afrika Kusini na kote barani Afrika ikifungiwa ufadhili.

Nchi nyingine ambazo zilikuwa zinategemea pakubwa ufadhili wa Marekani zikiwemo Zambia, Nigeria, Burundi na Ivory Coast tayari zinapambana ili kukidhi mahitaji yao kwa kutumia uwezo wao wa ndani, alisema Bi Byanyima lakini akasisitiza kuwa wanachokitoa hakitaweza kufidia ufadhili wa Marekani.

(Chanzo: AP)

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

magonjwa ya wanawake13 hours ago

Madhara ya kuvurugika kwa homoni za kike (Hormonal Imbalance in women)

Kuvurugika kwa hormone au vichocheo ni nini? Kuvurugika kwa hormone au vichocheo hutokea pale mwili unapozalisha homoni kwa kiwango kikubwa...

Hospital22 hours ago

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery)

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery) Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma za kibingwa...

magonjwa ya watoto22 hours ago

Tatizo La Mtoto Kuzaliwa Kabla Ya Wakati wake(premature birth)

Tatizo La Mtoto Kuzaliwa Kabla Ya Wakati wake(premature birth) Maana ya mtoto njiti (Preterm Birth) Mtoto njiti ni mtoto anayezaliwa...

Afya News23 hours ago

Vifaa Tiba vya TSH.BILIONI 1.2 Kuimarisha huduma za dharura ya Uzazi na watoto wachanga

VIFAA TIBA VYA TSH.BILIONI 1.2 KUIMARISHA HUDUMA ZA DHARURA YA UZAZI NA WATOTO WACHANGA Na Mvuda Jaffer, WAF – Arusha...

Afya News4 days ago

Jukwaa la takwimu za afya barani Afrika kuanza rasmi Nairobi, Kenya

Jukwaa la takwimu za afya barani Afrika kuanza rasmi Nairobi, Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO),...

Patient Stories5 days ago

Glaucoma ilimnyang’anya uwezo wa kuona, lakini mikono yake ilimpa kusudi jipya la maisha

Glaucoma ilimnyang’anya uwezo wa kuona, lakini mikono yake ilimpa kusudi jipya la maisha Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50...

Stars Health5 days ago

Joe biden aeleza hali yake ya saratani ya tezi dume kwa Sasa

Aliyekuwa Rais wa Marekani, Joe Biden, ameeleza kuwa ugonjwa wa saratani ya tezi dume (Prostate Cancer) unaendelea kuathiri shughuli zake...

Story5 days ago

Baadhi ya Watu huweza kuishi kwa kulala muda mfupi sana

Baadhi ya Watu huweza kuishi kwa kulala muda mfupi sana Baadhi ya watu wanaweza kuishi vizuri kwa usingizi mfupi sana....

masikio5 days ago

Madhara ya Masikio kupiga kelele (tinnitus) ni yapi?

Madhara ya Masikio kupiga kelele (tinnitus) Masikio kupiga kelele ni tatizo la kiafya linalojulikana kitaalamu kama Tinnitus. Hali hii hutokea...

Utafiti6 days ago

Utafiti: Wanawake nchini Kenya wanazaa watoto wachache kadiri vifo vya wajawazito vinavyoendelea kuwa changamoto

Utafiti mpya wa afya ya uzazi nchini Kenya umeonesha kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa na mwanamke mmoja imeendelea kupungua, huku...