Connect with us

magonjwa

Tatizo la Down Syndrome,chanzo,dalili na Tiba

Doctor Ombeni

Published

on

121 Views
0 Comments

Down Syndrome ni hali ya kinasaba (genetic disorder) ambayo hutokea mtoto anapozaliwa akiwa na nakala ya ziada ya kromosomu namba 21. Hii inasababisha matatizo mbalimbali ya kimwili, kiakili, na maendeleo ya mtoto.

Kwa kawaida, binadamu wana kromosomu 46 (23 kutoka kwa mama, 23 kutoka kwa baba), lakini mtoto mwenye Down Syndrome huwa na kromosomu 47 kwa kuwa kuna nakala ya ziada ya kromosomu namba 21 (hii inajulikana kama trisomy 21).

DALILI ZA UGONJWA WA DOWN SYNDROME NI PAMOJA NA;

1. Mtoto kuzaliwa na shingo fupi sana kuliko kawaida

2. Mtoto kuzaliwa na uso bapa pamoja na pua

3. Mtoto kuzaliwa na masikio madogo sana kuliko kawaida

4. Mtoto kuzaliwa na shida ya ulimi kutokeza nje

5. Mtoto kuzaliwa na mikono pamoja na miguu midogo sana

6. Mtoto kuzaliwa na vijinukta vyeupe kwenye sehemu nyeusi ya jicho

7. Mtoto kuzaliwa mfupi sana kuliko kawaida

8. Mtoto kuzaliwa na viganja vya mikono vikiwa na mstari mmoja tu.

Dalili za Down Syndrome kwa Watoto,Soma Zaidi hapa chini.

Dalili hutofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine, lakini mara nyingi huwa ni:

  • Uso wa kipekee (facial features):
    • Uso wa mviringo au bapa (flat face)
    • Macho yake kuangalia upande wa juu au pembeni(upslanting eyes)
    • Pua ndogo na mdomo mdogo
    • Masikio madogo au ya tofauti kimuundo
    • Ulimi ambao mara nyingine hutoka nje
  • Kuchelewa kwa ukuaji wa akili na mwili:
    • Kiwango cha akili kuwa cha chini kuliko kawaida (mild to moderate intellectual disability)
    • Kuchelewa kujifunza kutembea, kuongea, au kujifunza vitu vingine vya maendeleo kwa Mtoto
  • Misuli kuwa dhaifu (hypotonia) hasa wakiwa wachanga
  • Mikono yenye alama ya kipekee kwenye viganja (single palmar crease)
  • Shingo fupi na kichwa kidogo
  • Urefu wa mwili kuwa chini ya wastani kwa umri husika.

Magonjwa Yanayohusiana na Down Syndrome

Watoto wenye Down Syndrome wako kwenye hatari kubwa ya:

  • Matatizo ya moyo (congenital heart defects)
  • Shida za kusikia na kuona
  • Matatizo ya mfumo wa chakula (mfano duodenal atresia)
  • Matatizo ya tezi ya thyroid
  • Maambukizi ya mara kwa mara
  • Udhaifu wa misuli (hypotonia) unaoweza kusababisha matatizo ya misuli na mifupa n.k.

Chanzo Kikuu cha Down Syndrome

Chanzo kikuu ni kosa la mgawanyiko wa seli wakati wa kutungwa kwa mimba (nondisjunction), ambapo husababisha nakala ya ziada ya kromosomu 21. Hili si kosa la mzazi wala haliathiriwi na tabia ya wazazi isipokuwa:

  • Umri mkubwa wa mama: Hii huongeza Hatari, Fahamu hatari ya kuza mtoto wa aina hii huweza kuongezeka zaidi mama anapokuwa na umri wa miaka 35 na kuendelea.
  • Historia ya kupata mtoto mwenye Down Syndrome hapo kabla.

Je, Down Syndrome Inatibika?

Hakuna tiba ya kuondoa Down Syndrome. Hata hivyo, matibabu hufanyika kulingana na matatizo yanayojitokeza, ikiwemo:

  • Upasuaji wa matatizo ya moyo
  • Tiba ya fiziotherapia kwa misuli(Mazoezi)
  • Programu za elimu maalum kusaidia uwezo wa kujifunza
  • Dawa kwa matatizo ya tezi ya thyroid au mengineyo

Watoto wengi wenye Down Syndrome wakipata msaada mapema wanaweza kuishi maisha ya furaha na kujitegemea kiasi fulani.

Muhimu Kujua

✔ Down Syndrome siyo ugonjwa unaoambukiza
✔ Kila mtoto ni wa kipekee, wengine huathirika kidogo, wengine zaidi
✔ Mapenzi, msaada wa kifamilia, tiba sahihi na elimu ni muhimu sana

121 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Uzazi/Ujauzito3 hours ago

Mama mjamzito akiwa na mimba ya miezi 8 anaruhusiwa kusafiri safari ndefu ya masaa zaidi ya 24?

Mama mjamzito akiwa na mimba ya miezi 8 anaruhusiwa kusafiri safari ndefu ya masaa zaidi ya 24? Ndiyo, mama mwenye...

EVENTS4 hours ago

Siku ya Usalama wa Mgonjwa Duniani 2026: Huduma Salama kwa Magonjwa Yasiyoambukiza

Siku ya Usalama wa Mgonjwa Duniani (World Patient Safety Day) huadhimishwa kila mwaka tarehe 17 Septemba kwa lengo la kuongeza...

Hospital23 hours ago

MNH-Mloganzila Yafanya Upasuaji wa Kurekebisha na Kurefusha Mifupa kwa Mbinu ya Ilizarov

MNH-Mloganzila Yafanya Upasuaji wa Kurekebisha na Kurefusha Mifupa kwa Mbinu ya Ilizarov Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila imefanikiwa kufanya kwa...

EVENTS1 day ago

Wavunja Record ya Dunia kwa kupanda miche 2,51,446 kwa saa moja tu

Wavunja Record ya Dunia kwa kupanda miche 2,51,446 kwa saa moja tu. Katika juhudi kubwa za kushangaza kwenye kutunza mazingira,...

magonjwa ya wanawake1 day ago

Fangasi Ukeni: Chanzo na Dalili

Fangasi Ukeni: Chanzo na Dalili Fangasi ukeni ni maambukizi ya fangasi yanayotokea kwenye uke na mara nyingi husababishwa na fangasi...

magonjwa ya wanawake2 days ago

Hedhi yenye harufu mbaya: SABABU zinazoweza kusababisha

Kwa baadhi ya wanawake, damu ya hedhi inaweza kuwa na harufu fulani ambayo si sawa na harufu ya kawaida ya...

EVENTS2 days ago

Siku ya kuzuia kujiua duniani 2026: kubadili mtazamo na kuanza mazungumzo

SIKU YA KUZUIA KUJIUA DUNIANI 2026: KUBADILI MTAZAMO NA KUANZA MAZUNGUMZO Kaulimbiu ya 2026: “Changing the Narrative on Suicide” –...

Utafiti2 days ago

Vifo Vinavyotokana na Mimba kutunga Nje ya Kizazi

Mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy) ni hali ambayo mimba inajipandikiza nje ya sehemu ya kawaida ya kizazi,Mara nyingi...

Utafiti2 days ago

Ucheleweshaji wa huduma Ndani ya Hospitali Wawa Tishio Kubwa kwa Maisha ya Mama na Mtoto

Ucheleweshaji wa huduma ndani ya vituo vya afya umeonekana kuwa moja ya sababu kubwa zinazochangia vifo vya wajawazito na watoto...

Afya News3 days ago

Jinsi Dawa za Kulevya Zinavyoharibu Afya ya Kinywa na Meno

Matumizi ya dawa za kulevya yanaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili, ikiwemo ubongo, moyo, ini na mfumo wa fahamu. Hata...

122
0