magonjwa
Ugonjwa wa Appendix Au Kidole Tumbo,chanzo,dalili na Tiba
Ugonjwa wa Appendix Au Kidole Tumbo,chanzo,dalili na Tiba
Appendix au kidole tumbo ni sehemu ya muendelezo wa utumbo mkubwa au mpana mwishoni, ambapo huwa na kitu mithili ya kidole chako cha mwisho cha mkononi,
Mtu huweza kuwa na tatizo kwenye appendix, hali ambayo ikampelekea kuhitaji matibabu, mfano ni tatizo kama vile appendicitis.
Appendicitis- ni hali ambayo huhusisha appendix kuvimba na kujazwa na usaha, kisha kusababisha maumivu.
Dalili za Ugonjwa Wa Appendix Au Kidole Tumbo
Je, Ugonjwa Wa Appendix una dalili Zipi? Dalili za tatizo kwenye Appendix ni Pamoja na;
1. Kupata Maumivu ya ghafla ambayo huanza upande wa kulia mwa tumbo la chini
2. Kupata Maumivu ya ghafla ambayo huanza karibu na kitovu chako na mara nyingi huhamia kwenye tumbo lako la chini upande wa kulia
3. Kupata Maumivu ambayo huongezeka ikiwa unakohoa, kutembea au kufanya shughuli zingine
4. Kupata shida ya Kichefuchefu na kutapika
5. Kukosa hamu ya kula chakula
6. Kupata Homa ya kiwango cha chini(Low-grade fever) ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi ugonjwa unavyoendelea
7. Kupata tatizo la kujisaidia choo kigumu au kuharisha(Constipation or diarrhea)
8. Kuvimbiwa,tumbo kujaa gesi, Kuvimba kwa tumbo(Abdominal bloating) N.k
9. Kuwa na tatizo la gesi tumboni(Flatulence) n.k
Chanzo cha Ugonjwa Wa Appendix
Kwa kawaida baada ya chakula kuyeyushwa na umeng’enyaji kuendelea, kuna baadhi ya myeyusho wa chakula hupitia sehemu hii ya kidole tumbo au appendix.
Sasa endapo chakula kitapita hapa pamoja na vitu vidogo vidogo vigumu kama vile; mchanga N.K, vitu hivi haviwezi kupita hapa, hivo hujilundika hapa kila siku unapokula chakula kilichochanganyika na vitu hivi vigumu.
Hali hii huendelea hadi kufikia hatua ya kidole tumbo au appendix kuziba kwa juu pamoja na kuvimba na mtu kuanza kupata maumivu makali. Hapo ndipo chanzo cha tatizo la appendix huanza.
VIPIMO vya Ugonjwa wa Appendix
Vipo baadhi ya vipimo ambavyo huweza kufanyika kwa mtu mwenye dalili za ugonjwa wa appendix, na vipimo hivo ni kama vile;
- vipimo vya damu,
- ultrasound,
- Ct Scan N.K
Pia Mgonjwa anaweza kuchunguzwa dalili,historia ya ugonjwa pamoja na uchunguzi kwa njia ya kupapasa mikono ambayo hufanywa na mtaalam wa afya au dactari.
MATIBABU YA UGONJWA WA APPENDIX
– Matibabu ya ugonjwa wa appendix au kidole tumbo huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali katika hatua za mwanzoni za ugonjwa, lakini kama tatizo litaendelea mgonjwa atafanyiwa upasuaji na kuondoa kabsa hicho kidole tumbo.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
choo chenye makamasi
Choo chenye makamasi,chanzo cha kujisaidia choo chenye makamasi au Usaha
Choo chenye makamasi,chanzo cha kujisaidia choo chenye makamasi au Usaha
Chanzo au Sababu za Choo chenye makamasi au Usaha
- Maambukizi ya Bacteria au Parasite, ndyo mana ukiwa na Magonjwa kama Vile Amoeba unaweza kupata choo chenye vitu kama Kamasi.
Maambukizi ya vimelea kama vile Entamoeba histolytica,Salmonella, or Campylobacter huweza kusababisha hali hii.
- Maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Infections (STIs);Mfano wa magonjwa kama Chlamydia endapo yatashambulia eneo la haja kubwa(Rectal infection) huweza kusababisha hali ya kujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na Vitu kama Makamasi(Mucus) au Usaha.
- Kuwa na Jipu au Majibu kwenye eneo la haja kubwa, hii pia huweza kuchangia ukajisaidia kinyesi chenye vitu kama Makamasi au usaha
- Tatizo la Fistula Sehemu ya haja kubwa(Anal Fistula)
- Magonjwa ya uchochezi wa utumbo (Inflammatory Bowel Disease – IBD), (IBD),hapa nazungumzia hali kama vile Crohn’s disease pamoja na ulcerative colitis, ambayo yanaweza kusababisha makamasi kwenye choo, damu na maumivu ya tumbo.
- Ugonjwa wa Irritable Bowel Syndrome (IBS), ambapo baadhi ya wagonjwa hupata choo chenye makamasi hasa bila damu.
- Na Wakati mwingine mzio wa chakula(Allergy) au hali ya kutovumilia baadhi ya vyakula(Food Intolerance) inaweza pia kuongeza ute kwenye choo.
Nini cha kufanya ukiwa nyumbani?
Nini unaweza kufanya Ukiwa nyumbani endapo unaona hali ya Usaha au Kamasi kwenye kinyesi chako?
1.Kunywa maji mengi Kila Siku
2.Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi zaidi(Fibers)
3.Wasiliana na Mtoa huduma wako wa afya
Ongea na Mtoa huduma wa afya Mapema endapo;
-Unatokwa na Usaha au Vitu kama Kamasi na haviishi
-Unapata maumivu ya Tumbo au Misuli ya tumbo kuvuta au kukaza sana
-Unaona Damu kwenye choo
-Unapata hali ya Homa
-Unaharisha,hasa mfululizo kwa zaidi ya Siku 3
-Unapata hali ya kichefuchefu na Kutapika
-Unapungua Uzito bila kujua Sababu ni nini?
Je,Unachangamoto hii? na Unahitaji Msaada zaidi?
Kwa Ushauri zaidi na Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.
Reference;
https://www.medicalnewstoday.com/articles/310101
https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/mucus-in-stool
Other Links;
Wikipedia – Mucus
https://en.wikipedia.org/wiki/Mucus
Wikipedia – Feces
https://en.wikipedia.org/wiki/Feces
Wikipedia – Ulcerative colitis
https://en.wikipedia.org/wiki/Ulcerative_colitis
Wikipedia – Crohn’s disease
https://en.wikipedia.org/wiki/Crohn%27s_disease
Merck Manual Consumer Version – Mucus in Stool
https://www.merckmanuals.com/home
MSD Manual Professional Version
https://www.msdmanuals.com/professional
NCBI Bookshelf
https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/
StatPearls (NCBI Bookshelf)
https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430892/
afyatips
Dalili za uric acid kuzidi mwilini,Fahamu hapa
Dalili za Uric Acid Kuzidi Mwilini, Ishara, Takwimu na Vyanzo vyake
Uric acid ni taka inayozalishwa mwilini baada ya kuvunjwa kwa kemikali zinazoitwa purines, ambazo hupatikana kwenye baadhi ya vyakula na pia hutengenezwa na mwili. Kwa kawaida, uric acid hutolewa kupitia figo kwa njia ya mkojo. Hata hivyo, kiwango chake kinapozidi (hyperuricemia), kinaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.
Takwimu duniani
- Tafiti zinaonyesha kuwa takriban asilimia 20 ya watu wazima duniani wana kiwango cha juu cha uric acid, ingawa wengi hawana dalili mwanzoni.
- Kati ya watu wenye uric acid nyingi, karibu asilimia 20–25 wanaweza kupata ugonjwa wa gout katika maisha yao.
- Ugonjwa wa gout unaathiri zaidi ya watu milioni 55 duniani, na idadi inaendelea kuongezeka kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha.
Dalili za uric acid kuzidi mwilini
1. Maumivu makali ya viungo
Dalili maarufu zaidi ni maumivu ya ghafla kwenye viungo, hasa kidole kikubwa cha mguu. Maumivu yanaweza kuwa makali kiasi cha kushindwa kutembea.
2. Kuvimba na wekundu wa kiungo
Kiungo huvimba, huwa chekundu na kuwa cha moto au kupata hali ya joto/kuhisi kuungua kutokana na mkusanyiko wa uric acid.
3. Kiungo kuwa kigumu kusogeza
Baada ya shambulio la gout, kiungo kichoathirika kinaweza kuwa kigumu kukunja au kunyoosha. Mfano Kidole cha Mguu au Kidole cha Mkono n.k.
4. Maumivu ya mara kwa mara hasa usiku
Mashambulizi mengi ya gout hutokea usiku na yanaweza kumwamsha mtu usingizini.
5. Vinundu chini ya ngozi (Tophi)
Kwa watu wenye uric acid nyingi kwa muda mrefu, hujitokeza vinundu vigumu kwenye vidole, masikioni, mikononi au kwenye viwiko.
6. Mawe kwenye figo(Kidney stones)
Uric acid nyingi inaweza kuathiri figo zako kwa njia mbali mbali ikiwemo kutengeneza mawe kwenye figo(kidney stones) na kusababisha:
- Maumivu makali ya mgongo au ubavu.
- Kukojoa Damu kwenye mkojo.
- Maumivu wakati wa kukojoa.n.k.
7. Kupungua uwezo wa figo kufanya kazi
Iwapo hali itaendelea bila matibabu, inaweza kuharibu figo polepole.
Nini husababisha uric acid kuongezeka?
- Kula nyama nyekundu kwa kiwango kikubwa na maini mara kwa mara.
- Kunywa pombe, hasa bia.
- Vinywaji vyenye sukari nyingi.
- Unene uliopitiliza.
- Kuwa na Ugonjwa wa figo.
- Kuwa na matatizo kama vile Kisukari na shinikizo la damu.
- Kutumia Baadhi ya dawa kama jamii ya diuretics.
Nani yuko kwenye hatari zaidi?
- Wanaume.
- Wanawake baada ya kukoma hedhi.
- Wenye historia ya gout kwenye familia.
- Watu wenye uzito mkubwa.
- Wenye magonjwa ya figo au kisukari.
Jinsi ya kupunguza uric acid
- Kunywa maji ya kutosha kila siku.
- Punguza nyama nyekundu na vyakula vyenye purines nyingi.
- Epuka pombe na vinywaji vyenye sukari nyingi.
- Punguza uzito ikiwa una uzito uliopitiliza.
- Fanya mazoezi mara kwa mara.
- Tumia dawa ulizoandikiwa na daktari ikiwa kiwango ni cha juu au una gout.
Bonus point;
Uric acid nyingi mwilini inaweza isiwe na dalili mwanzoni, lakini ikiachwa bila kudhibitiwa inaweza kusababisha gout, mawe kwenye figo na hata uharibifu wa figo. Ukipata maumivu makali ya viungo, hasa kwenye kidole kikubwa cha mguu, ni muhimu kufanyiwa vipimo na kuanza matibabu mapema.
Je,Unachangamoto hii? Kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane +255758286584.
Reference;
- World Health Organization (WHO): https://www.who.int
- MedlinePlus – Uric Acid: https://medlineplus.gov/uricacid.html
- Mayo Clinic – Gout: https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/gout
- Cleveland Clinic – Hyperuricemia: https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/17808-hyperuricemia-high-uric-acid-level
- National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases (NIDDK): https://www.niddk.nih.gov
- American College of Rheumatology: https://rheumatology.org
- Wikipedia – Uric acid: https://en.wikipedia.org/wiki/Uric_acid
magonjwa
Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa
Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa
Chanzo cha Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa
- Maambukizi ya Bacteria au Parasite, ndyo mana ukiwa na Magonjwa kama Vile Amoeba unaweza kupata choo chenye vitu kama Kamasi.
Maambukizi ya vimelea kama vile Entamoeba histolytica,Salmonella, or Campylobacter huweza kusababisha hali hii.
- Uwepo wa Inflammatory Bowel Disease (IBD),hapa nazungumzia hali kama vile Crohn’s disease pamoja na ulcerative colitis
- Tatizo la Fistula Sehemu ya haja kubwa(Anal Fistula)
- Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Infections (STIs);Mfano wa magonjwa kama Chlamydia endapo yatashambulia eneo la haja kubwa(Rectal infection) huweza kusababisha hali ya kujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na Vitu kama Makamasi(Mucus) au Usaha.
- Kuwa na Jipu au Majibu kwenye eneo la haja kubwa n.k.
Nini cha kufanya ukiwa nyumbani?
Nini unaweza kufanya Ukiwa nyumbani endapo unaona hali ya Usaha au Kamasi kwenye kinyesi chako?
1.Kunywa maji mengi Kila Siku
2.Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi zaidi(Fibers)
3.Wasiliana na Mtoa huduma wako wa afya
Ongea na Mtoa huduma wa afya Mapema endapo;
-Unatokwa na Usaha au Vitu kama Kamasi na haviishi
-Unapata maumivu ya Tumbo
-Unaharisha,hasa mfululizo kwa zaidi ya Siku 3
-Unapata hali ya kichefuchefu na Kutapika
-Misuli ya tumbo kuvuta au kukaza sana
-Unapungua Uzito bila kujua Sababu ni nini?
Je,Unachangamoto hii? na Unahitaji Msaada zaidi?
Kwa Ushauri zaidi na Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.
Reference;
https://www.medicalnewstoday.com/articles/310101
https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/mucus-in-stool
-
magonjwa2 years ago
Muwasho sehemu za siri kwa mwanaume chanzo chake
-
afya5 years agoCHANZO CHA TATIZO LA KUPASUKA MIGUU KWENYE KISIGINO(gaga)
-
Madhara ya mtoto kunywa maji machafu2 weeks ago
Madhara ya mtoto kunywa maji machafu au maji ya uzazi
-
Madhara ya mtoto kunywa maji machafu2 weeks ago
Madhara ya Mtoto Kunywa Maji Machafu: Dalili, Hatari na Namna ya Kumsaidia
-
Madhara ya Pombe1 week agoJE, POMBE hupunguza testosterone na Ubora wa mbegu za Kiume?
-
afya5 years agoDawa za Kukausha kidonda,kuzuia maambukizi Na SABABU za Kidonda Kutokupona Haraka
-
Afya News1 week agoDaktari amfanyia Upasuaji Mama kumtoa Mtoto ili kumfanyia upasuaji wa Uvimbe Kisha Kumrudisha tena tumboni
-
choo chenye makamasi1 week ago
Choo chenye makamasi,chanzo cha kujisaidia choo chenye makamasi au Usaha

.jpeg)