Connect with us

magonjwa

Ugonjwa wa Ngozi,Scabies,Soma hapa kufahamu

Published

on

Ugonjwa wa Ngozi,Scabies,Soma hapa kufahamu


Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo chanzo chake ni utitiri mdogo sana yaani tiny burrowing mite ambao hujulikana kama Sarcoptes scabiei.  Mtu hupata muwasho sana kwenye eneo ambalo utitiri huo umechimba.

Na wakati mwingine hali huwa mbaya Zaidi nyakati za Usiku ambapo Utitiri huu huhitaji kuchimba Zaidi.

Scabies inaambukiza na inaweza kuenea haraka kupitia mawasiliano ya karibu ya mtu na mtu katika familia, kikundi cha watoto, darasa la shule, nyumba ya uuguzi au gereza n.k. Kwa sababu upele huenea kwa urahisi, wahudumu wa afya mara nyingi hupendekeza kutibu familia nzima au watu wowote wa karibu.”

SCABIES: Makala 

Scabies, ni ugonjwa wa ngozi unaohusishwa na kuwasha na madoa madogo mekundu kwenye ngozi, yanayosababishwa na utitiri wa kuwasha(itchy mite).

Aina ya Utitiri huu yaani tiny burrowing mite hujulikana kwa kitaalam kama Sarcoptes scabiei.

Dalili za Scabies

DALILI ZA UGONJWA WA SCABIES NI PAMOJA NA;

– Mtu kupata muwasho sana kwenye ngozi yake, na sana sana muwasho huu huzidi sana wakati wa usiku

– Kuanza kupata upele kwenye ngozi

– Ngozi kuanza kuwa na madoa doa mekundu

– Na maeneo ya ngozi ambayo huweza kuathiriwa zaidi ni pamoja na;

• Kati kati ya vidole

• Eneo la kwapani

• Kuzunguka kiuno

• Kwenye mikono

• Chini ya miguu kwenye sole

• Kuzunguka maziwa au matiti

• Kwenye sehemu za siri za Mwanaume(Around the male genital area)

• Eneo la matakoni

• Kwenye magoti

• Na kwa upande wa watoto wadogo, sana sana hutokea kwenye kichwa(Scalp), viganja vya mikono pamoja na miguuni.

MATIBABU YA SCABIES

– Zipo njia mbali mbali za kutibu Ugonjwa huu wa Scabies pamoja na vitu vya kuzingatia na kufanya ukiwa nyumbani, ikiwemo swala la usafi wa mwili pamoja nguo zako,

Na kwa upande wa tiba huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali ikiwemo za kunywa au Cream za kupaka n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

choo chenye makamasi

Choo chenye makamasi,chanzo cha kujisaidia choo chenye makamasi au Usaha

Published

on

Choo chenye makamasi,chanzo cha kujisaidia choo chenye makamasi au Usaha

Kujisaidia Choo chenye makamasi huashiria nini? Ukiona Vitu kama Makamasi au usaha kwenye kinyesi chako unatakiwa kufuatilia hali hii kwani inaweza kuwa Ishara muhimu inayoonyesha kuna kitu hakipo sawa ndani ya mwili wako. Ni muhimu kutofautisha hili kwa kujua aina ya uchafu unaotoka sehemu ya haja kubwa na unaashiria nini.
Choo chenye makamasi (mucus) au kinachoonekana kuwa na vitu kama usaha si hali ya kawaida, hasa kama hutokea mara kwa mara au kinaambatana na damu, maumivu makali ya tumbo, homa au kuharisha.
Wakati mwingine kuwa na hali ya vitu kama Kamasi au mucus kwenye kinyesi chako inakupa taarifa muhimu juu ya afya ya mwili. Wako baadhi ya Watu huona hali ya kamasi yenye chembechembe za damu au nyeupe au njano hii inaweza kuwa dalili ya ugonjwa kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Na hali kama vile tatizo la kupata choo kigumu/kukosa choo(Constipation) au kuharisha zinaweza kuambatana na hali hii ya kamasi kwenye kinyesi. Lakini pia kamasi au kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa inaweza kuwa dalili ya magonjwa makubwa zaidi.
Mara nyingi Kujisaidia Choo chenye makamasi au Usaha inaonyesha mwitikio wa kinga mwili dhidi ya maambukizi flani, hali ya uvimbe, au jipu kwenye njia yako ya kumeng’enya chakula. 
Sasa tuangalie Vizuri Chanzo au Sababu KUU za Mtu kujisaidia choo chenye Makamasi;

Chanzo au Sababu za Choo chenye makamasi au Usaha

Sababu kubwa za hali hii ya kutokwa na Usaha au Vitu kama Makamasi kwenye haja kubwa ni pamoja na;
  • Maambukizi ya Bacteria au Parasite, ndyo mana ukiwa na Magonjwa kama Vile Amoeba unaweza kupata choo chenye vitu kama Kamasi.

Maambukizi ya vimelea kama vile Entamoeba histolytica,Salmonella, or Campylobacter huweza kusababisha hali hii.

  • Maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Infections (STIs);Mfano wa magonjwa kama Chlamydia endapo yatashambulia eneo la haja kubwa(Rectal infection) huweza kusababisha hali ya kujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na Vitu kama Makamasi(Mucus) au Usaha.
  • Kuwa na Jipu au Majibu kwenye eneo la haja kubwa, hii pia huweza kuchangia ukajisaidia kinyesi chenye vitu kama Makamasi au usaha 
  • Tatizo la Fistula Sehemu ya haja kubwa(Anal Fistula)
  • Magonjwa ya uchochezi wa utumbo (Inflammatory Bowel Disease – IBD), (IBD),hapa nazungumzia hali kama vile Crohn’s disease pamoja na ulcerative colitis, ambayo yanaweza kusababisha makamasi kwenye choo, damu na maumivu ya tumbo.
  • Ugonjwa wa Irritable Bowel Syndrome (IBS), ambapo baadhi ya wagonjwa hupata choo chenye makamasi hasa bila damu.
  • Na Wakati mwingine mzio wa chakula(Allergy) au hali ya kutovumilia baadhi ya vyakula(Food Intolerance) inaweza pia kuongeza ute kwenye choo.

Nini cha kufanya ukiwa nyumbani?

Nini unaweza kufanya Ukiwa nyumbani endapo unaona hali ya Usaha au Kamasi kwenye kinyesi chako?

1.Kunywa maji mengi Kila Siku

2.Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi zaidi(Fibers)

3.Wasiliana na Mtoa huduma wako wa afya

Ongea na Mtoa huduma wa afya Mapema endapo;

-Unatokwa na Usaha au Vitu kama Kamasi na haviishi

-Unapata maumivu ya Tumbo au Misuli ya tumbo kuvuta au kukaza sana

-Unaona Damu kwenye choo

-Unapata hali ya Homa

-Unaharisha,hasa mfululizo kwa zaidi ya Siku 3

-Unapata hali ya kichefuchefu na Kutapika

-Unapungua Uzito bila kujua Sababu ni nini?

Je,Unachangamoto hii? na Unahitaji Msaada zaidi?

Kwa Ushauri zaidi na Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.

Reference;

https://www.medicalnewstoday.com/articles/310101

https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/mucus-in-stool

Other Links;

Wikipedia – Mucus
https://en.wikipedia.org/wiki/Mucus
Wikipedia – Feces
https://en.wikipedia.org/wiki/Feces
Wikipedia – Ulcerative colitis
https://en.wikipedia.org/wiki/Ulcerative_colitis
Wikipedia – Crohn’s disease
https://en.wikipedia.org/wiki/Crohn%27s_disease
Merck Manual Consumer Version – Mucus in Stool
https://www.merckmanuals.com/home
MSD Manual Professional Version
https://www.msdmanuals.com/professional
NCBI Bookshelf
https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/
StatPearls (NCBI Bookshelf)
https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430892/

Continue Reading

afyatips

Dalili za uric acid kuzidi mwilini,Fahamu hapa

Published

on

Dalili za Uric Acid Kuzidi Mwilini, Ishara, Takwimu na Vyanzo vyake

Uric acid ni taka inayozalishwa mwilini baada ya kuvunjwa kwa kemikali zinazoitwa purines, ambazo hupatikana kwenye baadhi ya vyakula na pia hutengenezwa na mwili. Kwa kawaida, uric acid hutolewa kupitia figo kwa njia ya mkojo. Hata hivyo, kiwango chake kinapozidi (hyperuricemia), kinaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.

Takwimu duniani

  • Tafiti zinaonyesha kuwa takriban asilimia 20 ya watu wazima duniani wana kiwango cha juu cha uric acid, ingawa wengi hawana dalili mwanzoni.
  • Kati ya watu wenye uric acid nyingi, karibu asilimia 20–25 wanaweza kupata ugonjwa wa gout katika maisha yao.
  • Ugonjwa wa gout unaathiri zaidi ya watu milioni 55 duniani, na idadi inaendelea kuongezeka kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha.

Dalili za uric acid kuzidi mwilini

1. Maumivu makali ya viungo

Dalili maarufu zaidi ni maumivu ya ghafla kwenye viungo, hasa kidole kikubwa cha mguu. Maumivu yanaweza kuwa makali kiasi cha kushindwa kutembea.

2. Kuvimba na wekundu wa kiungo

Kiungo huvimba, huwa chekundu na kuwa cha moto au kupata hali ya joto/kuhisi kuungua kutokana na mkusanyiko wa uric acid.

3. Kiungo kuwa kigumu kusogeza

Baada ya shambulio la gout, kiungo kichoathirika kinaweza kuwa kigumu kukunja au kunyoosha. Mfano Kidole cha Mguu au Kidole cha Mkono n.k.

4. Maumivu ya mara kwa mara hasa usiku

Mashambulizi mengi ya gout hutokea usiku na yanaweza kumwamsha mtu usingizini.

5. Vinundu chini ya ngozi (Tophi)

Kwa watu wenye uric acid nyingi kwa muda mrefu, hujitokeza vinundu vigumu kwenye vidole, masikioni, mikononi au kwenye viwiko.

6. Mawe kwenye figo(Kidney stones)

Uric acid nyingi inaweza kuathiri figo zako kwa njia mbali mbali ikiwemo kutengeneza mawe kwenye figo(kidney stones) na kusababisha:

  • Maumivu makali ya mgongo au ubavu.
  • Kukojoa Damu kwenye mkojo.
  • Maumivu wakati wa kukojoa.n.k.

7. Kupungua uwezo wa figo kufanya kazi

Iwapo hali itaendelea bila matibabu, inaweza kuharibu figo polepole.

Nini husababisha uric acid kuongezeka?

  • Kula nyama nyekundu kwa kiwango kikubwa na maini mara kwa mara.
  • Kunywa pombe, hasa bia.
  • Vinywaji vyenye sukari nyingi.
  • Unene uliopitiliza.
  • Kuwa na Ugonjwa wa figo.
  • Kuwa na matatizo kama vile Kisukari na shinikizo la damu.
  • Kutumia Baadhi ya dawa kama jamii ya diuretics.

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

  • Wanaume.
  • Wanawake baada ya kukoma hedhi.
  • Wenye historia ya gout kwenye familia.
  • Watu wenye uzito mkubwa.
  • Wenye magonjwa ya figo au kisukari.

Jinsi ya kupunguza uric acid

  • Kunywa maji ya kutosha kila siku.
  • Punguza nyama nyekundu na vyakula vyenye purines nyingi.
  • Epuka pombe na vinywaji vyenye sukari nyingi.
  • Punguza uzito ikiwa una uzito uliopitiliza.
  • Fanya mazoezi mara kwa mara.
  • Tumia dawa ulizoandikiwa na daktari ikiwa kiwango ni cha juu au una gout.

Bonus point;

Uric acid nyingi mwilini inaweza isiwe na dalili mwanzoni, lakini ikiachwa bila kudhibitiwa inaweza kusababisha gout, mawe kwenye figo na hata uharibifu wa figo. Ukipata maumivu makali ya viungo, hasa kwenye kidole kikubwa cha mguu, ni muhimu kufanyiwa vipimo na kuanza matibabu mapema.

Je,Unachangamoto hii? Kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane +255758286584.

Reference;

Continue Reading

magonjwa

Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa

Published

on

Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa

Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa huashiria nini? Ukiona usaha halisi, au Vitu kama kamasi nene, ya manjano/nyeupe iliyochanganywa na kinyesi chako, mara nyingi inaonyesha mwitikio wa kinga mwili dhidi ya maambukizi, hali ya uvimbe, au jipu kwenye njia yako ya kumeng’enya chakula n.k. Ni muhimu kutofautisha hili kwa kujua aina ya uchafu unaotoka sehemu ya haja kubwa na unaashiria nini.
Wakati mwingine ni kawaida kuwa na hali ya Kamasi(mucus) kwenye kinyesi chako. Lakini kamasi yenye chembechembe za damu au nyeupe au njano inaweza kuwa dalili ya ugonjwa kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Na hali kama vile tatizo la kupata choo kigumu/kukosa choo(Constipation) au kuharisha zinaweza kusababisha kamasi kwenye kinyesi. Lakini pia kamasi au kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa inaweza kuwa dalili ya magonjwa makubwa. zaidi.

Chanzo cha Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa

Sababu kubwa za hali hii ya kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa ni pamoja na;
  • Maambukizi ya Bacteria au Parasite, ndyo mana ukiwa na Magonjwa kama Vile Amoeba unaweza kupata choo chenye vitu kama Kamasi.

Maambukizi ya vimelea kama vile Entamoeba histolytica,Salmonella, or Campylobacter huweza kusababisha hali hii.

  • Uwepo wa Inflammatory Bowel Disease (IBD),hapa nazungumzia hali kama vile Crohn’s disease pamoja na ulcerative colitis
  • Tatizo la Fistula Sehemu ya haja kubwa(Anal Fistula)
  • Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Infections (STIs);Mfano wa magonjwa kama Chlamydia endapo yatashambulia eneo la haja kubwa(Rectal infection) huweza kusababisha hali ya kujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na Vitu kama Makamasi(Mucus) au Usaha.
  • Kuwa na Jipu au Majibu kwenye eneo la haja kubwa n.k.

Nini cha kufanya ukiwa nyumbani?

Nini unaweza kufanya Ukiwa nyumbani endapo unaona hali ya Usaha au Kamasi kwenye kinyesi chako?

1.Kunywa maji mengi Kila Siku

2.Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi zaidi(Fibers)

3.Wasiliana na Mtoa huduma wako wa afya

Ongea na Mtoa huduma wa afya Mapema endapo;

-Unatokwa na Usaha au Vitu kama Kamasi na haviishi

-Unapata maumivu ya Tumbo

-Unaharisha,hasa mfululizo kwa zaidi ya Siku 3

-Unapata hali ya kichefuchefu na Kutapika

-Misuli ya tumbo kuvuta au kukaza sana

-Unapungua Uzito bila kujua Sababu ni nini?

Je,Unachangamoto hii? na Unahitaji Msaada zaidi?

Kwa Ushauri zaidi na Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.

Reference;

https://www.medicalnewstoday.com/articles/310101

https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/mucus-in-stool

Continue Reading

Trending

Copyright © 2017 Zox News Theme. Theme by MVP Themes, powered by WordPress.