Connect with us

Afya News

Ukeketaji kwa watoto bado ni tatizo wasema kina mama Gambia

Doctor Ombeni

Published

on

Hulay Damba,ni mama mwenye umri wa miaka 55, kwa miaka mingi akitekeleza vitendo vya ukeketaji au FGM kwa wasichana katika jamii yake huko Basse, Gambia. 

Jukumu lake kama ngariba lalirithi kutoka kwa nyanya yake. “Ndivyo nilivyofundishwa,” ameeleza. Licha ya miaka ya juhudi za uhamasishaji nchini Gambia, viwango vya ukeketaji wa wanawake na wasichana bado ni vya juu, hata kwa vizazi vya sasa. 

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021, za Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA karibu robo tatu ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 wamekeketwa nchini Gambia kiwango ambacho ni sawa na kile cha wanawake wa kizazi kilichowatangulia wenye umri wa miaka 45 hadi 49.

Utafiti wa akina mama uliofanywa pia unaonesha matokeo yenye mchanganyiko wakati wanawake wenye mabinti wenye umri wa miaka 25 na chini ya  hapo waliulizwa kama mabinti wao wamekeketwa asilimia 54 walisema hapana.

Lakini asilimia 22 walisema kwamba binti zao sio tu wamekeketwa  bali walikeketwa kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja.

Kubadilisha mawazo

Nchini Gambia, wasichana wengi wanaokeketwa hukatwa sehemu zao za siri  wakati wa taratibu hizo za kijadi. Takriban asilimia 12 hushonwa kabisa. 

Karibu wote hupitia ukeketaji huu mikononi mwa wakunga wa jadi na mangariba kama Bi. Damba.

Bi. Damba amewahi kupata kipato kizuri cha msimu kwa kufanya kazi ya ungariba. “Niliamini ilikuwa ni heshima,” amelieleza shirika la UNFPA.

Yote yamebadilika miaka sita iliyopita, alipoanza kuhudhuria mafunzo kadhaa yaliyoongozwa na shirika lisilo la kiserikali la Tostan kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Italia (AICS) kupitia UNFPA, kuhusu madhara ya muda mrefu ya ukeketaji  ambayo yanaweza kujumuisha kutokwa na damu nyingi, maambukizi, na hata kifo.

“Kwa kutazama ya nyuma, natamani ningejua kile ninachojua sasa,” anasema Bi. Damba.

Leo hii, Bi Damba anaongoza  harakati za kukomesha  kazi hiyo ya ukeketaji pamoja na akina mama wenzake na vijana.

“Sasa natumia sauti yangu kuelimisha,” anasema, “kwa sababu kila msichana anastahili kukua akiwa salama na kamili.”

Madhara katika wakati wa kujifungua

Fatou amezungumza na UNFPA akiwa katika wodi ya uzazi kwenye Hospitali ya Wilaya ya Basse. Akiwa na miaka 16 tu, akimshika mtoto mchanga wa kike mikononi mwake, akiugua kutoka katika kujifungua  kwa ugumu  baada ya kukeketwa. 

Ujauzito wake ulihatarisha maisha yake na ya mtoto wake. Kwa bahati nzuri, mkunga aliweza kuingilia kati na kumsaidia. Hili ni jambo ambalo linajulikana kuongeza kwa kiasi kikubwa hatari za uzazi.

Hospitali hiyo ni sehemu ya mtandao unaokua wa vituo vya afya vinavyoshiriki katika mpango wa UNFPA, unaofadhiliwa na mradi wa AICS, kwa msaada wa ziada kutoka China Aid, unaotoa mafunzo maalum kwa watoa huduma za afya ili kushughulikia madhara ya ukeketaji, pamoja na huduma nyingine muhimu za afya ya uzazi.

Hata hivyo, bado hatua zaidi zinahitajika.

Mwaka jana, wabunge walijaribu  bila mafanikio kuhalalisha ukeketaji wa wanawake, ambao umepigwa marufuku nchini Gambia tangu mwaka 2015. Wasichana, wakiwemo watoto wachanga, bado wanakumbwa na ukeketaji na kupata madhara yake.

Si ajabu kuwa ukeketaji hufanywa na wanawake wakubwa, anasema Fatou Baldeh, mwanzilishi wa shirika la Women in Liberation and Leadership. 

“Wanawake bado ni waathirika na pia watekelezaji wa mila hii yenye ukatili mkubwa inayojaa ubaguzi wa kijinsia,” anasema. 

“Wanawake hawa si watendaji tu ni matokeo ya mfumo unaofundishwa tangu kuzaliwa kwamba maumivu na kujitoa mhanga ni sehemu ya kuwa mwanamke shupavu.”

Kile kinachohitajika, ameongeza, ni juhudi za “kubomoa mienendo inayowasukuma wanawake kutekeleza kitendo hiki.”

Sasa kizazi kipya cha wanaharakati kinainuka kupambana na hali hiyo. Ramata Baldeh, msichana mwenye umri wa miaka 18, alikeketwa akiwa mdogo  lakini anasema ukeketaji utaishia kwake.

“Ikiwa nitapata binti siku moja, sitaruhusu kamwe apitie mateso niliyopitia,” anasema. “Nataka aende shule ili aweze kutimiza ndoto zake na  achague njia yake mwenyewe.” Via UN.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

magonjwa ya wanawake13 hours ago

Madhara ya kuvurugika kwa homoni za kike (Hormonal Imbalance in women)

Kuvurugika kwa hormone au vichocheo ni nini? Kuvurugika kwa hormone au vichocheo hutokea pale mwili unapozalisha homoni kwa kiwango kikubwa...

Hospital21 hours ago

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery)

Muhimbili kufanya upasuaji wa kurejesha nguvu za kiume (Penile Implant Surgery) Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeendelea kuboresha huduma za kibingwa...

magonjwa ya watoto22 hours ago

Tatizo La Mtoto Kuzaliwa Kabla Ya Wakati wake(premature birth)

Tatizo La Mtoto Kuzaliwa Kabla Ya Wakati wake(premature birth) Maana ya mtoto njiti (Preterm Birth) Mtoto njiti ni mtoto anayezaliwa...

Afya News22 hours ago

Vifaa Tiba vya TSH.BILIONI 1.2 Kuimarisha huduma za dharura ya Uzazi na watoto wachanga

VIFAA TIBA VYA TSH.BILIONI 1.2 KUIMARISHA HUDUMA ZA DHARURA YA UZAZI NA WATOTO WACHANGA Na Mvuda Jaffer, WAF – Arusha...

Afya News4 days ago

Jukwaa la takwimu za afya barani Afrika kuanza rasmi Nairobi, Kenya

Jukwaa la takwimu za afya barani Afrika kuanza rasmi Nairobi, Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO),...

Patient Stories5 days ago

Glaucoma ilimnyang’anya uwezo wa kuona, lakini mikono yake ilimpa kusudi jipya la maisha

Glaucoma ilimnyang’anya uwezo wa kuona, lakini mikono yake ilimpa kusudi jipya la maisha Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50...

Stars Health5 days ago

Joe biden aeleza hali yake ya saratani ya tezi dume kwa Sasa

Aliyekuwa Rais wa Marekani, Joe Biden, ameeleza kuwa ugonjwa wa saratani ya tezi dume (Prostate Cancer) unaendelea kuathiri shughuli zake...

Story5 days ago

Baadhi ya Watu huweza kuishi kwa kulala muda mfupi sana

Baadhi ya Watu huweza kuishi kwa kulala muda mfupi sana Baadhi ya watu wanaweza kuishi vizuri kwa usingizi mfupi sana....

masikio5 days ago

Madhara ya Masikio kupiga kelele (tinnitus) ni yapi?

Madhara ya Masikio kupiga kelele (tinnitus) Masikio kupiga kelele ni tatizo la kiafya linalojulikana kitaalamu kama Tinnitus. Hali hii hutokea...

Utafiti6 days ago

Utafiti: Wanawake nchini Kenya wanazaa watoto wachache kadiri vifo vya wajawazito vinavyoendelea kuwa changamoto

Utafiti mpya wa afya ya uzazi nchini Kenya umeonesha kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa na mwanamke mmoja imeendelea kupungua, huku...