Connect with us

magonjwa

Kuhisi vitu vinatembea mwilini,chanzo chake na Tiba

Doctor Ombeni

Published

on

Kuhisi vitu vinatembea mwilini,chanzo chake na Tiba

Hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini kwa kitaalam hujulikana kama Formication

Baadhi ya watu hupatwa na shida hii ya kuhisi kama kuna Vitu vinatembea Mwilini Kila wakati,

Je chanzo chake ni nini?

Chanzo cha Kuhisi vitu vinatembea mwilini

Zipo Sababu mbali mbali ambazo huchangia hali hii,na baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na hizi:

1. Ugonjwa wa brucella:

Kwa Asilimia Kubwa hizi ni dalili za Ugonjwa wa Brucella

Ugonjwa wa Brucella ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Brucellosis na chanzo chake kikubwa ni maambukizi ya Bacteria wanaojulikana kama BRUCELLA,

Bacteria hawa hutoka kwa wanyama mbali mbali kama vile; Ng’ombe, mbuzi,kondoo,Nguruwe,Mbwa n.k,

Baadhi ya dalili zake ni:

  • Mgonjwa kupatwa na homa ambazo hujirudia mara kwa mara
  • Mgonjwa kuhisi kama vile kuna vitu vinatembea mwilini mwake, na wakati mwingine huhisi kama minyoo wakati wa kujisaidia haja kubwa
  • Mgonjwa kuanza kutetemeka mwili baada ya kuhisi baridi kali au kuwa na Homa
  • Mgonjwa kupoteza kabsa hamu ya kula chakula au kitu chochote
  • Mwili kuchoka Sana
  • Kupata maumivu ya Viungo,joint n.k.

2. Matatizo kwenye mfumo wa Neva(Neurological conditions):

Kwa Mtu mwenye ugonjwa wowote unaoathiri utendaji kazi wa Neva anaweza kupata dalili hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini, Mfano ni magonjwa kama vile;

  •  Ugonjwa wa kisukari ambao husababisha hali inayoitwa diabetic neuropathy n.k.

3. Kuwa na matatizo katika afya ya Akili:

Wakati mwingine ukiwa na Msongo wa mawazo mkubwa,Hofu sana,au hali zingine zinazohusu afya ya akili unaweza kupata dalili hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini,

4. Matumizi ya baadhi ya Dawa:

Zipo baadhi ya dawa ukitumia unaweza kupata hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini,

5. Matatizo ya Ngozi(Skin conditions):

Yapo baadhi ya matatizo ya ngozi kama vile;

  • Tatizo la ngozi kuwa kavu(Dry skin),
  • Mzio kwenye ngozi(Skin allergic reactions),
  • Au matatizo kama scabies wakati mwingine huweza kusababisha hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini,

6. Upungufu wa Virutubisho mwilini(Nutritional deficiencies):

Baadhi ya tafiti zinaonyesha,Kuwa na kiwango kidogo cha madini kama vile magnesium au upungufu wa Vitamini B mwilini huweza kuchangia pia dalili hii ya  Kuhisi vitu vinatembea mwilini,

7. Mabadiliko ya Vichocheo mwilini(Hormonal changes):

Mfano kwa Baadhi ya Wanawake wakifika kipindi cha ukomo wa hedhi(menopause) hupata mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini, hali ambayo huweza kuchangia dalili hii pia ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini.

8. Tatizo la Minyoo;

Pia Minyoo(real parasitic worms) pamoja na hali za Ngozi(Skin conditions) kama nilivyoeleza hapo juu huweza kusababisha muwasho wa ngozi,hali kama ya ngozi kuchoma choma au kuhisi kama Vitu vinatembea chini ngozi.

Je,Unachangamoto hii na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti23 hours ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka Vinavyosababishwa na Magonjwa ya Moyo na Kiharusi – Utafiti...

Afya News1 day ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo vitatu vyaripotiwa wiki hii Mtoto mchanga nchini Marekani amefariki dunia...

CHANJO1 day ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola zinatarajiwa kuongezwa kwenye...

Afya News2 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke. Bodi ya Dawa na Sumu...

magonjwa2 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA NINI? Mikono kufa ganzi ni hali ambayo mtu hupoteza hisia...

Uzazi&Ujauzito3 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti5 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...

afyatips5 days ago

Upungufu wa Vitamini D,Dalili Zake, Visababishi na Madhara Ambayo Unaweza Usiyatambue Mapema

Patient Story Via BBC;Sikujua nilikuwa na upungufu wa vitamini D hadi nilipozirai kazini’ Msichana mwenye umri wa miaka 23, Saskia...