Connect with us

Afya ya Akili

Wanasaikolojia watoa ‘tiba’ utulivu wa akili kwa hivi sasa,nini cha kufanya

Doctor Ombeni

Published

on

109 Views
0 Comments

WANASAIKOLOJIA nchini wameshauri jamii kutafuta utulivu wa kiakili kwa kutoka nje ya makazi yao ili kukutana na watu wengine na kuona namna hali ya usalama ilivyorejea jambo litakalowasaidia kuwa sawa kiakili.

Mwanasaikolojia kutoka Chama cha Wanasaikolojia Tanzania (TAPA), Jesusa Malewo amewashauri watu watembee hadi kwenye maeneo ambayo walikuwa wanayaogopa ili kuona kile wanachofikiri hakipo na wakubaliane na hali ilivyo sasa.

Amewasihi wazungumze na watu mara kwa mara na kila mmoja afanye utambuzi kwa mwenzie ili kubaini kama tabia zao zimebadilika kwa ajili ya kuwasaidia kurejea katika hali ya mwanzo.

“Baadhi ya watu walishuhudia watu wakipoteza maisha, wapo ambao wameharibiwa mali na biashara zao, hivyo kutokana na hali hiyo baadhi yao wamepata majeraha ya kihisia, tatizo linaloweza kuwafanya wakumbuke mara kwa mara na kuwapa kiwewe kwa sababu utendaji kazi wa mfumo wa akili umebadilika ghafla,” amesema Malewo.

Ameeleza kuwa kuna watu waliopata msongo wa mawazo na huzuni, hawawezi kuwa salama kutokana na hali hiyo, hivyo kila mmoja anapaswa kuzungumza na watu tofauti kwa kutafakari namna ya kuanza maisha mapya na kuachana na yaliyopita ili kila mmoja awe na uwezo wa kusonga mbele kwa kasi bila kukwamishwa na matukio ya hapo awali.

“Mtu ambaye hakupitia changamoto yoyote hawezi kutambua maumivu ya wale walikumbwa na matatizo katika vurugu hizo, sasa kila mmoja wetu anapaswa kuvaa kiatu cha mwingine na kubebea tatizo lake kwa ajili ya kujua namna ya kusaidiana ili wasahau yaliyowakumba,” amesema.

Ametoa wito kwa wadau wa saikolojia na serikali kuchukulia uzito suala hilo ili watu wapate msaada na waepuke

magonjwa wanayoweza kuwapata kutokana na kuwa na hofu.

Malewo aliishauri serikali kuweka mikakati ya wananchi kupatiwa elimu ya saikolojia mara kwa mara na kufanya tathmini ya watu walioathirika kisaikolojia kutokana na vurugu hizo ili wapatiwe msaada kabla hawajapata madhara makubwa zaidi ambayo yanaweza kuwasababishia magonjwa.

“Ni muhimu watu kujengewa uwezo wa kujiimarisha kabla hayo mambo hayajatokea, wapewe elimu ya udhibiti wa msongo wa mawazo na kukabiliana na majanga ya dharura ili waweze kukabiliana na kumudu hali zote, kukabiliana na hisia na kujenga ujasiri wakati wote,” amesema.

Ametoa wito kwa viongozi wa serikali na Watanzania kuacha matumizi ya kauli za maudhi pamoja na kutopuuzia kauli zinazotolewa na watu.

Naye mwanasaikolojia, John Ambrose amewashauri Watanzania kuepuka kutumiana ujumbe na taarifa za vitisho na matukio yaliyotokea hapo awali kwa sababu wanaweza kusababisha hofu zaidi inayoweza kuwasababishia magonjwa yanayotokana na matatizo ya ubongo.

“Kila mmoja meathirika kwa namna ya tofauti, sasa inatakiwa watu wajipatie msaada kwanza wao wenyewe kwa kujipa tafsiri nzuri kwamba tatizo lililotokea limekwisha na wasijifungie ndani, watembee ili waone maisha yamerudi kama hapo awali na waonane wa watu wengine kwa ajili ya kubadilishana mawazo,” amesema Ambrose.

Ameeleza ni vyema jamii ikaongeza ushirikiano zaidi kimawazo, kiuchumi na kijamii kwa kuwa tatizo hilo halikuwa na maandalizi, hakuna mtu aliyejiandaa na wapo waliokuwa hawana uwezo wa kupata mahitaji muhimu ikiwemo chakula.

“Kitendo cha watu kukaa ndani kimewaathiri baadhi ya watu kibishara, ndoto na mipango ya watu kwa sababu

baadhi yao hutumia mitandao kufanya shughuli zao za uchumi, kupata furaha na kuondoa upweke,” amesema.

109 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

Hospital7 hours ago

MNH-Mloganzila Yafanya Upasuaji wa Kurekebisha na Kurefusha Mifupa kwa Mbinu ya Ilizarov

MNH-Mloganzila Yafanya Upasuaji wa Kurekebisha na Kurefusha Mifupa kwa Mbinu ya Ilizarov Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila imefanikiwa kufanya kwa...

EVENTS9 hours ago

Wavunja Record ya Dunia kwa kupanda miche 2,51,446 kwa saa moja tu

Wavunja Record ya Dunia kwa kupanda miche 2,51,446 kwa saa moja tu. Katika juhudi kubwa za kushangaza kwenye kutunza mazingira,...

magonjwa ya wanawake10 hours ago

Fangasi Ukeni: Chanzo na Dalili

Fangasi Ukeni: Chanzo na Dalili Fangasi ukeni ni maambukizi ya fangasi yanayotokea kwenye uke na mara nyingi husababishwa na fangasi...

magonjwa ya wanawake1 day ago

Hedhi yenye harufu mbaya: SABABU zinazoweza kusababisha

Kwa baadhi ya wanawake, damu ya hedhi inaweza kuwa na harufu fulani ambayo si sawa na harufu ya kawaida ya...

EVENTS1 day ago

Siku ya kuzuia kujiua duniani 2026: kubadili mtazamo na kuanza mazungumzo

SIKU YA KUZUIA KUJIUA DUNIANI 2026: KUBADILI MTAZAMO NA KUANZA MAZUNGUMZO Kaulimbiu ya 2026: “Changing the Narrative on Suicide” –...

Utafiti1 day ago

Vifo Vinavyotokana na Mimba kutunga Nje ya Kizazi

Mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy) ni hali ambayo mimba inajipandikiza nje ya sehemu ya kawaida ya kizazi,Mara nyingi...

Utafiti2 days ago

Ucheleweshaji wa huduma Ndani ya Hospitali Wawa Tishio Kubwa kwa Maisha ya Mama na Mtoto

Ucheleweshaji wa huduma ndani ya vituo vya afya umeonekana kuwa moja ya sababu kubwa zinazochangia vifo vya wajawazito na watoto...

Afya News2 days ago

Jinsi Dawa za Kulevya Zinavyoharibu Afya ya Kinywa na Meno

Matumizi ya dawa za kulevya yanaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili, ikiwemo ubongo, moyo, ini na mfumo wa fahamu. Hata...

magonjwa3 days ago

Ugonjwa wa Selimundu,dalili,chanzo na Tiba

Katika Makala hii tunachambua Zaidi kuhusu Dalili za ugonjwa wa seli mundu,chanzo cha ugonjwa wa Seli mundu pamoja na Matibabu...

Afya News3 days ago

Wataalam wa maabara wahimizwa kuboresha huduma za afya kwa Wananchi

WATAALAM WA MAABARA WAHIMIZWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI Na Zakayo Mosha- WAF Morogoro Wataalam wa Maabara wamehimizwa kutumia...

110
0