Uzazi/Ujauzito
Mjamzito Mapigo Ya Moyo Kwenda Mbio
Mjamzito Mapigo Ya Moyo Kwenda Mbio
Mapigo ya moyo kwenda mbio kwa mjamzito (moyo kudunda haraka) ni jambo linaloweza kutokea mara nyingi wakati wa ujauzito. Wakati mwingine ni kawaida, lakini wakati mwingine linaweza kuashiria tatizo.
Sababu za kawaida (zisizo hatari)
Hizi hutokana na mabadiliko ya mwili kipindi cha ujauzito:
- Kuongezeka kwa ujazo wa damu mwilini (Blood volume)(moyo hufanya kazi zaidi)
- Homoni za ujauzito
- Wasiwasi au msongo wa mawazo
- Uchovu au kukosa usingizi
- Kunywa kahawa/ chai nyingi au vinywaji vyenye caffeine
Sababu zinazoweza kuwa hatari
- Upungufu wa maji mwilini (dehydration)
- Upungufu wa damu (anemia)
- Kiwango cha sukari mwilini kuwa chini (low blood sugar)
- Shinikizo la juu la damu au preeclampsia
Muone daktari haraka kama kuna dalili hizi:
- Mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi sana na hayapungui,Dalili zinaendelea muda mrefu
- Kizunguzungu au kuzimia
- Maumivu ya kifua
- Kupumua kwa shida
- Mapigo yasiyo ya kawaida (kuruka-ruka)
- Kuvimba sana mwilini
- Homa
Nini cha kufanya nyumbani
- Kunywa maji ya kutosha
- Pumzika na lala ubavu wa kushoto
- Epuka kahawa nyingi na soda
- Kula milo midogo mara kwa mara
- Epuka joto kali na msongo
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa
.jpeg)
