Others
Tahadhari ya ujio wa tetemeko yatangazwa Japan baada ya kuondoa onyo la Tsunami
Tahadhari ya ujio wa tetemeko yatangazwa Japan baada ya kuondoa onyo la Tsunami
Maafisa nchini Japani wameonya kuhusu tetemeko la ardhi “kubwa” linalotarajiwa katika wiki ijayo baada ya tetemeko la ukubwa wa richa 7.7 kutokea pwani ya kaskazini-mashariki, na kusababisha amri ya kuhama na maonyo ya mawimbi ya tsunami ya mita 3 (futi 10).
Maelfu ya watu waliamuriwa kuondoka katika maeneo ya pwani kwenda kwenye maeneo ya juu baada ya tetemeko hilo katika karibu na mkoa wa Iwate, kilomita 530 (maili 330) kaskazini mwa mji mkuu Tokyo.
Mawimbi makubwa zaidi ya tsunami yalikuwa na urefu wa sentimita 80. Onyo la ujio wa Tsunami liliondolewa saa chache baada ya tetemeko hilo Jumatatu.
Lakini shirika la hali ya hewa la Japan limeonya kwamba matetemeko “yanayosababisha tetemeko kubwa zaidi” yanaweza kutokea katika wiki ijayo, na kusababisha mawimbi makubwa zaidi.
Mamlaka ilisema kuna uwezekano wa kutokea tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa richa 8.0 au zaidi kuliko wakati wa kawaida.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass, Kama unachangamoto yoyote ya kiafya; Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatsApp, Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaJapan ina kumbukumbu za tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mwaka 2011 lililosababisha tsunami iliyogharimu maisha ya zaidi ya watu 18,000 na kusababisha kuyeyuka kwa kinu cha nyuklia cha Fukushima. Via BCC.
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)