DAWA
Matumizi sahihi ya dawa ni yapi?
Imeboreshwa July 31, 2026 by Doctor Ombeni
Matumizi sahihi ya dawa ni yapi?
Hili ni Swali ambalo wafwatiliaji wengi wa afyaclass wamekuwa wakituuliza,na wengine huchanganyikiwa zaidi pale ambapo wanaambiwa;
Tumia Dawa,asubuh,mchana na Jion,
Tumia Dawa Asubuh na Jion
Tumia Dawa kutwa mara 3 n.k…
Haya ni maneno ambayo hutumika sana kwenye Dawa, Lakini je unaelewa maana yake?
Fahamu Matumizi Sahihi ya Dawa
Muda Sahihi wa kutumia Dawa ni kama ifuatavyo;
1.Ukiambiwa Kutwa mara 3
Ni kila baada ya Saa 8 unatumia dawa
2.Kutwa mara 2 ni kila baada ya Saa 12 unatumia dawa
3. Na kutwa mara 1 unatumia kila baada ya Saa 24.


