magonjwa
Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa
Imeboreshwa July 10, 2026 by Doctor Ombeni
Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa
Chanzo cha Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa
- Maambukizi ya Bacteria au Parasite, ndyo mana ukiwa na Magonjwa kama Vile Amoeba unaweza kupata choo chenye vitu kama Kamasi.
Maambukizi ya vimelea kama vile Entamoeba histolytica,Salmonella, or Campylobacter huweza kusababisha hali hii.
- Uwepo wa Inflammatory Bowel Disease (IBD),hapa nazungumzia hali kama vile Crohn’s disease pamoja na ulcerative colitis
- Tatizo la Fistula Sehemu ya haja kubwa(Anal Fistula)
- Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Infections (STIs);Mfano wa magonjwa kama Chlamydia endapo yatashambulia eneo la haja kubwa(Rectal infection) huweza kusababisha hali ya kujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na Vitu kama Makamasi(Mucus) au Usaha.
- Kuwa na Jipu au Majibu kwenye eneo la haja kubwa n.k.
Nini cha kufanya ukiwa nyumbani?
Nini unaweza kufanya Ukiwa nyumbani endapo unaona hali ya Usaha au Kamasi kwenye kinyesi chako?
1.Kunywa maji mengi Kila Siku
2.Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi zaidi(Fibers)
3.Wasiliana na Mtoa huduma wako wa afya
Ongea na Mtoa huduma wa afya Mapema endapo;
-Unatokwa na Usaha au Vitu kama Kamasi na haviishi
-Unapata maumivu ya Tumbo
-Unaharisha,hasa mfululizo kwa zaidi ya Siku 3
-Unapata hali ya kichefuchefu na Kutapika
-Misuli ya tumbo kuvuta au kukaza sana
-Unapungua Uzito bila kujua Sababu ni nini?
Je,Unachangamoto hii? na Unahitaji Msaada zaidi?
Kwa Ushauri zaidi na Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.
Reference;
https://www.medicalnewstoday.com/articles/310101
https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/mucus-in-stool


