Ebola
Wagonjwa 5 wapona Ugonjwa wa Ebola,WHO yasema
Wagonjwa 5 wapona Ugonjwa wa Ebola,WHO yasema
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilisema kwenye taarifa yake ya Jumapili (Mei 31) kwamba wagonjwa wengine zaidi wanatazamiwa kupona, hasa pale ugunduzi na matibabu yanapoanza mapema, huku juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo hatari zikiongezeka.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mfanyakazi mmoja wa maabara aliyekuwa ameambukizwa, alipona ugonjwa huo na hivyo kuifanya idadi ya waliopona kufikia watano.
Nje ya Afrika, wagonjwa wachache wanaendelea kutibiwa nchini Brazil na Italia, baada ya kupata maambukizo wakitokea mataifa yaliyokumbwa na ugonjwa huo.
Idadi ya watu waliokwishaambukizwa nchini Kongo imefikia 282, ambapo 42 wamepoteza maisha.
WHO iliitangaza aina mpya ya kirusi cha Bundibugyo kuwa sababu ya mripuko wa sasa wa Ebola ndani ya Kongo na Uganda, ambako kumetangazwa hali ya dharura ya kiafya lakini bado haijafikia kiwango cha kuwa janga. via Dw.
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa
.jpeg)