Patient Stories
Apoteza Watoto watano aliojifungua kabla ya muda (njiti)
Simanzi imetawala kwa familia ya Karen Remi (22) ambaye ni Mkazi wa Arusha baada ya kupoteza Watoto wake watano aliojifungua kabla ya muda (njiti) katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.
Kwa mujibu wa taarifa, Karen alijifungua Watoto hao akiwa na ujauzito wa miezi sita (wiki 26) ambapo wote walifariki dunia kwa nyakati tofauti kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati na kila mmoja kuwa na uzito wa chini ya kilo moja.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Karen amesema alikuwa amejiandaa kwa furaha kuwapokea Watoto hao, lakini mambo yamekuwa tofauti na matarajio yake.
Kwa upande wake, Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, Simforosa amesema Mama huyo alipata uchungu kabla ya wakati akiwa na ujauzito wa wiki 26.
Ameeleza kuwa Watoto wote walizaliwa njiti na walikuwa na uzito wa chini ya kilo moja kila mmoja, hali iliyopunguza uwezekano wao wa kuendelea kuishi.
“Watoto watano ni wengi, Mama alitakiwa kupumzika zaidi na Watoto walizaliwa wakiwa na uzito wa chini ya kilo moja kila mmoja,” amesema Simforosa.
Credits: MillardAyoUPDATES
