Afya News
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imewasha vifaa vya usikivu (Cochlear Implant) kwa watoto saba
Imeboreshwa August 2, 2026 by Doctor Ombeni
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imewasha vifaa vya usikivu (Cochlear Implant) kwa watoto saba waliopandikizwa vifaa hivyo.
Tangu kuzinduliwa kwa huduma hiyo mwaka 2017, jumla ya wagonjwa 115 wamefanyiwa upasuaji wa kupandikizwa vifaa hivyo hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Bw. Emmanuel Tayari, ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuweka mikakati ya kusogeza huduma mbalimbali za kibobezi karibu na wananchi.
Lengo kuu ni kupunguza changamoto za kiafya zinazoweza kuepukika na kupunguza mzigo wa gharama za matibabu kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Dellilah Kimambo, ameeleza kuwa gharama za matibabu hayo nchini sasa ni TZS milioni 45, ikilinganishwa na TZS milioni 120 zilizokuwa zikitumika kwa mgonjwa mmoja aliyetumwa nje ya nchi.
Aliongeza kuwa kuwapandikiza watoto vifaa hivyo mapema kunawawezesha kusikia na kuepuka uziwi, jambo linalowapa fursa ya kusoma na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii.
‎credits: ITV.
