Utafiti
Nchi 15 Zenye Mifumo Mibovu Zaidi ya Huduma za Afya Duniani mwaka 2026
Imeboreshwa July 25, 2026 by Doctor Ombeni
Utafiti wa mwaka 2026 unaotokana na Numbeo Health Care Index, uliokusanywa na Visual Capitalist, umeonyesha kuwa bado kuna mataifa mengi yanayokabiliwa na changamoto kubwa katika utoaji wa huduma za afya. Ripoti hiyo inategemea maoni ya wananchi kuhusu ubora wa huduma wanazopata katika nchi zao.
Kwa mujibu wa tathmini hiyo, Belarus ndiyo nchi iliyoorodheshwa kuwa na mfumo mbovu zaidi wa huduma za afya kati ya nchi zilizotathminiwa katika kundi la mwisho, ikiwa na alama 50 kati ya 100.
Nafasi ya pili kutoka mwisho inashikiliwa na Ireland, iliyopata alama 51, jambo linaloonyesha kuwa hata baadhi ya mataifa yenye uchumi mkubwa bado yanakabiliwa na malalamiko kuhusu huduma za afya.
Nchi za Cambodia, Serbia na Moldova zilipata alama sawa za 52, huku Iran na Malta zikipata 53.
Katika nafasi zinazofuata, Trinidad and Tobago pamoja na Hungary zilipata alama 54, wakati Algeria, Bosnia and Herzegovina, na North Macedonia zilifungana kwa alama 55.
Aidha, Ukraine na Georgia zilipata alama 56, huku Romania ikifunga orodha ya nchi 15 za mwisho kwa alama 57.
Orodha ya nchi 15 zenye mifumo mibovu zaidi ya afya mwaka 2026
- Belarus – Alama 50
- Ireland – Alama 51
- Cambodia – Alama 52
- Serbia – Alama 52
- Moldova – Alama 52
- Iran – Alama 53
- Malta – Alama 53
- Trinidad and Tobago – Alama 54
- Hungary – Alama 54
- Algeria – Alama 55
- Bosnia and Herzegovina – Alama 55
- North Macedonia – Alama 55
- Ukraine – Alama 56
- Georgia – Alama 56
- Romania – Alama 57
Vigezo vilivyotumika
Ripoti hii haikupima idadi ya hospitali au matumizi ya serikali pekee, bali ilitathmini maoni ya wananchi kuhusu huduma wanazopokea. Mambo yaliyopimwa ni pamoja na:
- Uwezo na weledi wa wahudumu wa afya.
- Ubora wa hospitali na miundombinu ya matibabu.
- Ubora wa huduma za matibabu kwa ujumla.
- Gharama za kupata huduma za afya.
- Kuridhika kwa wananchi na mfumo wa afya nchini mwao.
Matokeo haya yanaonyesha kuwa wananchi katika nchi hizo wanaridhishwa kwa kiwango cha chini na huduma za afya kutokana na changamoto zinazohusisha ubora wa huduma, miundombinu, upatikanaji wa wataalamu na gharama za matibabu.
Chanzo: The Star Kenya; Numbeo Health Care Index 2026; Visual Capitalist.
