Connect with us

magonjwa

Ugonjwa wa ngozi kuwasha chanzo na Tiba

Doctor Ombeni

Published

on

Imeboreshwa July 26, 2026 by Doctor Ombeni

Ugonjwa wa Ngozi Kuwasha (Pruritus): Sababu, Dalili, Tiba na Njia za Kujikinga

Ngozi Kuwasha (Pruritus) ni hali inayomfanya mtu ahisi hamu kubwa ya kujikuna. Watu wengi hudhani ni ugonjwa wenyewe, lakini kwa kweli kuwashwa kwenye ngozi ni dalili inayoweza kusababishwa na magonjwa mbalimbali ya ngozi au matatizo yanayotokea ndani ya mwili.

Takwimu za Kimataifa

  • Utafiti uliohusisha watu 50,552 kutoka nchi 20 uligundua kuwa takribani 39.8% ya watu walikuwa wamepata tatizo la ngozi kuwasha ndani ya kipindi kilichochunguzwa. Afrika ilikuwa na kiwango cha juu zaidi (45.7%).
  • Ngozi kuwasha ni miongoni mwa sababu zinazowafanya mamilioni ya watu kutafuta huduma za kitabibu kila mwaka duniani kote.

Sababu za Ngozi kuwasha

Hali ya Ngozi Kuwasha Inaweza kusababishwa na:

  • Tatizo la Ngozi kukauka sana(dry skin).
  • Tatizo la Mzio (allergy) dhidi ya Vitu mbali mbali.
  • Maambukizi kwenye damu(Blood Infection)
  • Tatizo la Minyoo
  • Ugonjwa wa Pumu ya ngozi au Eczema (Atopic dermatitis).
  • Fangasi wa ngozi.
  • Muwasho Mkali kwenye ngozi na Upele unaotokana na tatizo la scabies.
  • Kuumwa na wadudu.
  • Psoriasis.
  • Magonjwa yanayohusu ini.
  • Hali ya nyongo kuzidi mwilini
  • Magonjwa yanayohusu figo.
  • Ugonjwa wa Kisukari.
  • Matatizo ya tezi (thyroid).
  • Baadhi ya dawa.
  • Matatizo ya neva.
  • Na kwa baadhi ya Watu wakiwa kwenye hali ya Msongo wa mawazo huweza kukutana na changamoto hii pia

Dalili ambazo unaweza kuzipata

Dalili zinaweza kujumuisha:

  • Kuwasha sehemu moja au mwili mzima.
  • Kupata Upele kwenye ngozi
  • Ngozi kuwa nyekundu.
  • Hali ya ngozi kuvimba
  • Ngozi kukauka na kupasuka.
  • Vipele au malengelenge.
  • Michubuko kutokana na kujikuna.
  • Kukosa usingizi kutokana na kuwashwa usiku.

Scabies: Sababu Mojawapo ya Muwasho Mkali kwenye ngozi

Scabies husababishwa na kimelea kidogo kinachochimba ndani ya ngozi na husababisha kuwasha sana, hasa usiku.

Kwa mujibu wa WHO:

  • Zaidi ya watu milioni 200 duniani huathirika na scabies wakati wowote.
  • Zaidi ya watu milioni 400 hupata scabies kila mwaka.

Tiba ya Tatizo la ngozi kuwasha

Matibabu hutegemea chanzo cha tatizo.

Daktari anaweza kupendekeza:

  • Krimu za kulainisha ngozi ikiwa imekauka.
  • Dawa za kupunguza mzio (antihistamines).
  • Krimu za corticosteroid kwa baadhi ya magonjwa ya ngozi.
  • Dawa za kuua fangasi ikiwa ni fangasi.
  • Dawa maalumu za scabies ikiwa chanzo ni upele huo.
  • Kutibu ugonjwa wa msingi kama kisukari, ugonjwa wa ini au figo ikiwa ndiyo chanzo.

Njia za Kujikinga

  • Oga kwa maji yasiyo ya moto sana.
  • Tumia sabuni laini.
  • Paka mafuta au moisturizer mara baada ya kuoga.
  • Epuka kujikuna.
  • Vaa nguo zisizokera ngozi.
  • Tumia dawa kwa ushauri wa mtaalamu.
  • Dumisha usafi wa mwili na mazingira.
  • Kwa scabies, hakikisha watu wote wa karibu wanatibiwa kwa wakati mmoja ili kuzuia maambukizi kurudi.

Ni Lini Umwone Daktari?

Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya ikiwemo wa afyaclass ikiwa:

  • Kuwasha kunaendelea zaidi ya wiki mbili bila sababu kujulikana.
  • Muwasho ni Mkali sana kiasi cha kukuzuia kulala.
  • Unapata homa.
  • Ngozi imevimba sana.
  • Unapungua uzito bila sababu.
  • Ngozi na macho vinakuwa vya njano.
  • Kuwasha kunasambaa mwili mzima bila upele unaoonekana.

Kumbuka;

Kuwasha ngozi si ugonjwa mmoja bali ni dalili inayoweza kuashiria tatizo la ngozi au ugonjwa wa ndani ya mwili. Kupata uchunguzi sahihi au kuongea na Wataalam wa afya ni muhimu ili kutibu chanzo badala ya kupunguza kuwasha pekee.

Je,Unasumbuliwa na Changamoto hii,Kwa USHAURI&TIBA tuwasiliane +255758286584.

Reference;

WHO

American Academy of Dermatology (AAD)

PubMed

NCBI (PMC)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass.Hapa utapata Ushauri & Tiba juu ya magonjwa mbali mbali. Kwa msaada Zaidi Tuwasiliane kupitia namba: +255758286584.Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *