Hospital
Akamatwa hospitali kwa kujifanya Mtoa Roho
Akamatwa hospitali kwa kujifanya Mtoa Roho
Mwanamume mwenye umri wa miaka 26 nchini Wales amekamatwa baada ya mamlaka kusema alipanda juu ya paa la hospitali akiwa amevaa mavazi yanayofanana na “Grim Reaper” (Mtoa Roho) na akasimama kimya akiwaangalia wagonjwa, wageni na wafanyakazi kwa karibu saa moja.
Polisi wanasema Leon Gillespie alisimama juu ya lango la kuingilia hospitali akiwa amevaa vazi jeusi lenye kofia na akiwa ameshika kitu kilichoonekana kama upanga mrefu. Polisi na wazima moto walifika eneo la tukio, na hali hiyo ilidumu kwa takribani dakika 50 kabla ya kumkamata.
Baadaye, Gillespie alikiri kosa la kusababisha usumbufu kwenye eneo la hospitali bila sababu ya msingi. Hata hivyo, mahakamani hakutoa maelezo yoyote kuhusu kwa nini alivaa mavazi hayo au kwa nini alipanda juu ya paa la hospitali.
✍️: #TRIGGAH (@officialtriggah )
