Story
Furaha Chilambo wa Mtwara Mikindani, ajifungua watoto watano kwa wakati mmoja
Furaha Chilambo wa Mtwara Mikindani, ajifungua watoto watano kwa wakati mmoja
Furaha Chilambo, mwenye umri wa miaka 32 na mkazi wa Kata ya Mtawanya, Mtaa wa Mangamba, Manispaa ya Mtwara Mikindani, amejifungua watoto watano kwa wakati mmoja katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini – Mtwara.
Furaha na mume wake, Said Hamisi, wamepokea kwa furaha ujio wa watoto hao, ambao ni mmoja wa kike na wanne wa kiume, na kufanya jumla ya watoto wao kufikia saba.
Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini, Dkt. Harry Mwambe, Furaha alijifungua Agosti 7, 2026, kwa ushirikiano wa jopo la madaktari, wakunga na wahudumu wengine wa afya.
Naye Mkunga Bobezi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini, Cresensia Mlelwa, amesema ujauzito wa watoto watano ulikuwa na changamoto, lakini kutokana na juhudi, weledi na ushirikiano wa madaktari, wakunga na wauguzi, mama huyo amefanikiwa kujifungua salama.

Amesema kwa sasa hali ya afya ya mama na watoto hao inaendelea kuimarika.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass,Kama unachangamoto yoyote ya kiafya;Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatSapp,Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaPamoja na furaha ya kupata watoto hao watano, Furaha na mume wake wameomba Serikali, taasisi mbalimbali, wadau wa maendeleo na wananchi wenye moyo wa kusaidia kuwafikia na kuwasaidia katika malezi ya watoto hao.
Wamesema mahitaji ya kulea watoto saba ni makubwa ikilinganishwa na kipato chao, hivyo wanaomba msaada wa mahitaji muhimu kwa watoto pamoja na mtaji utakaowawezesha wazazi hao kufanya shughuli za kiuchumi na kugharamia mahitaji ya familia.
Medical Disclaimer
Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa